MCHOME AKAGUA UTOAJI WA MSAADA WA KISHERIA MKOANI SINGIDA

  • Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome atembelea mkoa wa Singida kukagua utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi.
  • Prof Mchome yuko katika ziara ya ukaguzi wa huduma na maeneo yanayotolewa msaada wa kisheria ili kuona kama inaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Kisheria No 1. ya 2017.
KM
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma ya msaada wa sheria mkoani Singida alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya ukaguzi.
  • Katika ziara hiyo Prof. Mchome ambaye ameambatana na Msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria nchini bibi Felistas Mushi, amezungumza na wanufaika wa huduma ya msaada wa kisheria katika mkoa wa Singida ambao wameelezea kuridhishwa kwako na huduma hiyo ambayo wamesema imewezesha kutatua matatizo yaliyokuwa yakiwakabili na hivyo kupata haki zao.
  • Ziara hiyo ya ukaguzi ni utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria No.1 ya 2017 ambayo inamtaka msimamizi wake kuvitembelea vituo vinavyotoa huduma ya msaada wa kisheria ili kuona maeneo wanakotolea huduma na aina y ahuduma wanayoitoa kwa mujibu wa sheria hiyo.

KM

  • Akizungumza na watoa msaada kutoka wilaya za Singida, Iramba, Mkalama Prof. Mchome amewataka kuzingatia kuwa msaada wa kisheria ni huduma muhimu ambayo wananchi wanahitaji kupewa kwa kuwa sio kila mwananchi anao ufahamu wa sheria.
  • Amewataka kuhakikisha wanatoa msaada wa kisheria ili kuwawezesha wananchi kutatua matatizo yanayowakabili na hivyo kuokoa muda ambao wangeutumia kujishughulisha kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

KM

  • Amesema matatizo mengi yanatatuliwa na sheria mbalimbali na ndio maana mtu akipata mtaalamu wa sheria anakuwa amepata njia sahihi na salama ya kutatua tatizo lake na kuokoa muda kwani atakuwa amerahisisha mambo mengi.
  • “Sheria ni kama uzio ambao una milango inayotakiwa kufunguliwa  ili kuweza kujua njia sahihi ya kupita na kupitia msaada wa kisheria mtaweza kuwaonyesha njia sahihi wananchi wenye shida na hivyo kutatua matatizo yao,” alisema Prof. Mchome na kuongeza kuwa sheria zikitumiwa vizuri huleta jamii zenye amani na furaha nakufanya jamii hizo kupata maendeleo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUPELEKA MAWASILIANO YA SIMU SINGIDA MASHARIKI

Serikali imeahidi kujenga mnara wa simu katika Kijiji cha Msule kilichopo kata ya Misugha jimbo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *