Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya wanyama Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA IKULU YA PRETORIA NCHINI AFRIKA KUSINI

RAIS
Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa akisikiliza maelezo yaliokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu vitabu hivyo vya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Mei, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa, Ikulu Jijini Pretoria.
  • Katika Mazungumzo hayo, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Rais Ramaphosa kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amemhakikishia kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria na nchi hiyo ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Nelson Mandela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ANC (African National Congress).
 
RAIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
  • Mhe. Rais Magufuli amemshukuru, Mhe. Rais Ramaphosa kwa kumkaribisha kufanya nae mazungumzo siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amebainisha kuwa anatarajia uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini utaimarishwa zaidi katika masuala ya uchumi na kukuza lugha ya Kiswahili.
  • Kwa upande wake, Mhe. Rais Ramaphosa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake, na amemhakikishia kuwa Afrika Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika ukombozi wa Taifa hilo na kwamba katika kipindi chake cha uongozi wake atauendeleza na kuuza zaidi uhusiano huo.
RAIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
  • Mhe. Rais Ramaphosa amesema kufuatia uamuzi wa Afrika Kusini kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo katika shule za msingi na sekondari.
  • Aidha, Mhe. Rais Ramaphosa ameahidi kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Tanzania kabla ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliopangwa kufanyika mwezi Agosti 2019 nchini Tanzania. Na pia atahudhuria mkutano huo.
RAIS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wakifurahia jambo katika mazungumzo yao Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
  • Kabla ya mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemkabidhi Mhe. Rais Ramaphosa zawadi ya vitabu vya kusoma na kufundishia lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  • Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Ramaphosa wamefanya mazungumzo hayo ikiwa ni kabla Mhe. Rais Ramaphosa hajatangaza Baraza lake la Mawaziri.
  • Mhe. Rais Magufuli kesho ataondoka nchini Afrika Kusini na kuelekea nchini Namibia ambako atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob.
 
Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Pretoria 
26 Mei, 2019
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

4 Maoni

  1. Very interesting subject, regards for posting.!

  2. Having read this I believed it was very enlightening. I appreciate you finding the time and effort to put this informative article together. I once again find myself spending way too much time both reading and posting comments. But so what, it was still worth it.

  3. I blog often and I seriously thank you for your content. This article has truly peaked my interest. I am going to take a note of your site and keep checking for new details about once per week. I opted in for your RSS feed as well.

  4. I needed to thank you for this wonderful read!! I certainly enjoyed every little bit of it. I have you saved as a favorite to look at new things you post…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *