- Waziri wa Nchini Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angellah Kairuki amebainisha mkakati maalum wa serikali kupitia utekelezaji wa BLUE PRINT wenye lengo la kuondoa vikwazo na changamoto zinazozuia ukuaji wa uwekezaji na urahisi wa kufanya biashara nchini.
- Mkakati huo unapendekeza,pamoja na mambo mengine,marekebisho ya sheria mbalimbali,kuondoa urasimu na uratibu mzuri wa Mamlaka za Udhibiti bila kuleta usumbufu kwa Wawekezaji.
- Kairuki ameyasema hayo jana katika Hotel ya Coral Beach,Dar es salaam wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uingereza (British Business Group) kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji hao na kuahidi kuzitatua kwa hatua mbalimbali kwa kushirikiana na Taasisi za serikali ili kuifanya Tanzania sehemu nzuri ya uwekezaji.
- Aidha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde amewashukuru Wawekezaji hao kwa kuendelea kutengeneza nafasi za Ajira kwa Watanzania kupitia Uwekezaji wao ambapo takribani Watanzania 300,000 wameajiriwa kupitia uwekezaji uliofanywa na Kampuni za Kutoka Uingereza nchini lakini pia amewataka wawekezaji hao kuzingatia sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini na Sheria ya Uratibu wa Ajira kwa wageni wakati wa uendeshaji wa shughuli zao hapa nchini.
- Akitoa salamu za Shukrani,Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali wito wa kukutana na wawekezaji wao ili kusikiliza changamoto zao na kuahidi kuwa bega kwa bega na serikali katika kusaidia utekelezaji wa mkakati wa kuondoa vikwazo katika uwekezaji nchini Tanzania.
Ad