CRDB BENKI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUWEZESHA MITAJI KWA WAJASIRIAMALI VIJANA

MV
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndg Majid Nsekela
  • Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Majid Nsekela ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa inayofanya katika kuleta maendeleo na kuwahudumia Watanzania na hivyo katika kuunga mkono juhudi za serikali Benki ya CRDB ipo tayari kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha mitaji wajasiriamali Vijana kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji ili kukuza uchumi wa kijana mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
  • Majid Nsekela ameyasema hayo leo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki ya CRDB Azikiwe,Dar es salaam wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde juu ya namna bora ya kukuza mitaji ya wajasiriamali Vijana nchini Tanzania.
MV-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndg Majid Nsekela
  • Akitoa maelezo yake,Naibu Waziri Mavunde ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuamua kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha Vijana kupitia mikopo ya masharti nafuu katika kuendeleza Uchumi wa Viwanda na kuahidi kutoa ushirikiano ili azma hii ya kuwafikia Vijana wengi zaidi nchini ikamilike kama ambavyo matarajio ya Serikali yanavyoainisha kwamba ifikapo mwaka 2025 takribani 40% ya nguvu kazi nchini iwe imeajiriwa kwenye sekta ya Viwanda.
Ad

Unaweza kuangalia pia

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI KATIKA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.