WANANCHI CHIBOLI KUFURAHIA SIKUKUU YA EID EL-FITR NA UMEME

  • Wananchi katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, Jimbo la Mtera, watasherehekea sikukuu ya Eid El-fitr wakiwa na umeme kwa mara ya kwanza, baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kuwasha umeme katika Kijiji hicho.
  • Akiwa ameambatana Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga,  Naibu Waziri wa Nishati, amewasha umeme katika Zahanati ya Kijiji hicho pamoja na Kisima cha Maji ambapo Kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa BTIP (kV 400) ambao umesambaza umeme katika Vijiji 121 vinavyopitiwa na mradi kutoka Iringa hadi Shinyanga.
UM
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto kwa Naibu Waziri), Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga (kulia kwa Naibu Waziri) wakishangilia mara baada ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino.
  • Akizungumza na Wananchi, Mgalu alisema kuwa, kuwashwa kwa umeme katika Kijiji hicho ni muendelezo wa utekelezaji wa adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano kufikisha umeme katika Vijiji vyote nchini.
  • Amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mwaka 2015 kulikuwa vijiji takribani 2,018 vyenye umeme ambapo kuanzia Januari 2016, vijiji vipya vilivyoongezeka ni takribani 5000 hivyo hadi sasa vijiji 7,290 vina umeme kati ya Vijiji 12,268.
UM
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho.
  • Kuhusu usambazaji umeme katika maeneo ambayo hayajapata umeme ingawa yamepitiwa na miundombinu alisema kuwa, kuna mradi wa ujazilizi, mzunguko wa Pili unaolenga kuongeza wigo wa kuunganisha umeme katika vitongoji mbalimbali na Dodoma ni kati ya Mikoa itakayoguswa na mradi huo.
  • Naibu Waziri, pia alisisitiza wananchi kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ambavyo vitawawezesha kuondokana na gharama za wiring na kuwezesha kuunga wateja wengi katika mradi huo wa BTIP.
UM
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho.
  • Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde alishukuru Serikali kwa kupeleka umeme katika Kijiji hicho, hata hivyo aliomba umeme huo ufike katika maeneo muhimu kama vile shamba la umwagiliaji, nyumba za ibada, na vitongoji vya Kijiji hicho.
UM
Zahanati katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino ambayo imepata umeme kupitia mradi wa BTIP (kV 400) uliosambaza umeme katika Vijiji 121 vinavyopitiwa na mradi huo kutoka Iringa hadi Shinyanga.
  • Aidha, aliipongeza Serikali kwa kufanya kazi bila ubaguzi kwani idadi ya watu katika Kijiji hicho si kubwa ukiliganisha na vijiji vingine lakini Serikali haikungalia idadi ya watu hao ili kufikisha umeme katika Kijiji hicho wala hadhi ya nyumba.
  • Wilaya ya Chamwino, ina vijiji 107 na vijiji 54 tayari vimesambaziwa umeme huku kazi ya usambazaji ikiendelea kupitia miradi mbalimbali kama REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza na BTIP.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.