Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Prof. Mohammed Janabi akiwa na Mkuu
wa Kitengo cha Matibabu ya Moyo kwa Watoto katika taasisi hiyo ambaye
pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa taasisi hiyo
Dkt. Naiz Majani wakibadilishana mawazo nje ya jengo la Kitengo cha
Matibabu ya Moyo kwa Watoto cha taasisi hiyo ambalo lilitolewa mwaka
jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli. Jengo hilo ambalo limemalizika kukarabatiwa mwezi uliopita
na tayari limeshaanza kupokea wagonjwa, lina vitanda 40 kwa ajili ya
watoto tu, na pia lina vitanda 8 kwa ajili ya wagonjwa mahututi (ICU)
kwa watoto tu na muda wowote kuanzia sasa litafunguliwa rasmi.
JENGO LA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO KUFUNGULIWA RASMI