MIRADI 15 YENYE THAMANI YA TSH. BILIONI 22.9 YAZINDULIWA WILAYANI ARUMERU

  • Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio za siku mbili katika halmashauri mbili za wilaya ya Arumeru ambapo jumla ya miradi 15 Kati ya Miradi 16 yenye thamani ya Bilioni 22.9 imezinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi, na mingine kukaguliwa na kuangalia uendelevu wake
  • Akihitimisha mbio hizo za mwenge kwa halmashauri ya Meru , kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 Ndugu Mzee Mkongea Ali mbali na kuridhishwa na ubora wa miradi ,amempongeza Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro kwa kuisimamia vizuri na kuhakikisha miradi hiyo inaleta tija kwa taifa
JR
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ,akiwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Alikwanza kulia.
  • Akizungumza katika mradi wa Maji wa Majengo wenye thamani ya shilingi milioni 754 ambao ulipaswa kuwekewa jiwe la msingi , kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali amesema mradi huo japo ni mzuri na umefikia katika hatua nzuri na kuanza kutoa huduma ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kuchukua hatua kali kwa aliekuwa mhandisi wa maji wa Halmashauri ya Meru ambae amehamishwa kwa kuidhinisha malipo ya shilingi milioni mbili (2,000,000)ambayo hayakufanya kazi iliyokusudiwa
JR
Mwenge wa Uhuru
  • Mkuu wa wilaya ya Arumeru amemshukuru Kiongozi wa mbio za mwenge 2019 pamoja na wakimbiza mwenge wengine ambapo amewahidi kuongeza kasi ya usimamiaji wa miradi mingine ambayo haikuwepo kwenye ratiba za mwenge ili pamoja nayo iweze kukamilika mapema na kuleta tija kwa taifa
  • Mwenge wa uhuru umendelea na mbio zake katika wilaya ya Arusha Jiji , kisha utakwenda Monduli na kumaliza mbio zake karatu kabla ya kukabidhiwa kwa mkoa wa Manyara siku ya Alhamisi

Imetolewa na ofisi ya mkuu wa wilaya Arumeru
10/06/2019

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI UMMY AZINDUA BODI YA TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameizindua Bodi ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *