ROTARY CLUB YAENDELEA KUWEKEZA SAME

SM 2-01

  • Rotary Club ya Same na Rotary club ya Ames Iowa – USA kuendelea kuwekeza katika miradi ya maji ili kuwezesha wananchi kupata maji safi na salama. Eng. Steve Jones na Eng. Dave Millard kutoka Iowa USA wamefika Same kufuatilia maendeleo ya mradi wa maji unaojengwa kata ya Mhezi kwa ufadhili wa club hiyo.
    Mradi utahudumia vijiji vitatu vya Mhezi, Mteke na Mtunguja ambapo utagharimu Tshs. 1,300,000,000 mpaka utakapoisha.
  • Mradi huo ni wa tatu kujengwa na club hiyo katika Wilaya ya Same na kuwezesha watu 6350 Kupata maji. “Nyie ni marafiki wazuri kwa kuwa mnashirikiana na serikali kujua vipaumbele vyetu na ni wawazi kwa kila mnachokifanya. Tunaendelea kuwakaribisha kuifanya Same kuwa ya tofauti” Alisema DC – Same.
  • Ambapo aliwakabidhi Kalenda za Wilaya walizozinunua baada ya kuona picha ya Rotary katika miradi iliyopita. Pia walikabidhiwa tangawizi bora ya Same na kuombwa kushiriki utekelezaji wa mpango mkakati wa mazingira Wa Wilaya ya Same.
  • Rais wa Rotary Club Same aliwashukuru kwa kuendelea kutoa fedha na kukubali kufadhili vijiji vingine vitatu kwa miradi ya maji na huduma za afya.
Ad

Unaweza kuangalia pia

HOSPITALI YA MAWENZI YAWAFANYIA UPASUAJI WA JICHO WAGONJWA 640

Kufuatia maboresho mbalimbali katika Sekta ya Afya hapa Nchini Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.