SOKO LA MADINI LAFUNGULIWA RASMI ARUSHA

  • Waziri wa Madini Dotto Mashaka Biteko amezindua soko la madini mkoani Arusha ambalo litawarahisishia wafanyabiashara na kuruhusu mzunguko wa fedha jambo ambalo serikali imeamua kusimamia rasilimali za nchi
  • Akizungumza katika ufunguzi  wa soko hilo Biteko amesema hakuna serikali inayoweza kujiendesha bila kulipa kodi ambapo maendeleo ya nchi yanaletwa kwa kulipa kodi pesa hizo zipatikana kwenye madini na watu wa kufanya hivyo ni watanzania wenyewe.
BT
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akimsikiliza mmoja wawafanyabiashara wa madini ambao wanaongeza thamani na kutengeneza vito vya thamani alipokuwa anatembelea maonyesho ya bidhaa za madini katika ufunguzi wa soko la Madini mkoani Arusha.
  • Mhe. Biteko amesema jambo hilo ni la kwanza kutokea  kihistoria tangia kupata uhuru kuwa na soko la madini katika mkoa wa Arusha,kwani Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na madini ambapo mengine hayawezi kupatikana  nchi nyingine zaidi isipokuwa nchi ya Tanzania.
  • Amewataka wafanyabiashara wa madini kupambana kuondoa rushwa kwenye sekta ya madini na kuwasihi kutokutumia muda mwingi kuwashawishi kuchukua zawadi kwani kwa kufanya hivyo hakusaidii kuondoa rushwa kwenye sekta ya madini,ametoa tahadhari kwa watu wote ambao wanadhania soko hilo wanaweza wakalihujumu
BT
Waziri wa Madini Dotto Biteko akisalimiana na wafanyabiashara wa madini Mkoani Arusha katika ufunguzi wa soko la madini mkoani hapo.
  •  “WanaArusha wachukieni watu wanaokwepa kulipa kodi,wachukienu wanaotorosha madini na tumpende mtu anayelipa kodi  na sisi serikali mtu anayelipa kodi tumpe heshima akija kwenye ofisi yako mpe na maji ya kunywa.amesema Biteko” alisema Biteko
  • Mrisho Gambo ni mkuu wa mkoa wa Arusha amewataka wafanyabiashara hao kulitumia soko hilo kwa faida na amewajakikishia kuwa hakuna mfanyabiashara atakayenyang’anywa madini yake kama baadhi ya watu wanavyozusha,amesema yeye yupo tayari kushirikiana na Waziri katika wizara husika ,kuhakikisha hakuna mfanyabiashara wa madini ananyanyaswa.
  • ” Wapo baadhi ya watu wanakujakuja wanajifanya wao sijui nani sijui nini wanafanya mambo ya ajabu ajabu namba zetu mnazo malengo wa serikali siyo kunyanyasa wafanyabiashara ,lengo la serikali nikuwatengenezea mazingira mazuri ili ipate haki yake na nyie mpate haki yenu”alisema Gambo
BT
Wafanyabiashara wa madini
  • Aidha amemuomba mhe.Waziri kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani hapo, waruhusiwe kuwa na senta ya kisasa ya madini,waendelee kufanya maonyesho ya madini kwani mkoa huo ni wa kimataifa na unapata wageni wengi kutoka nchi za nje na Taasisi nyingi za Kimataifa,zipo mkoani hapo ambapo mkoa huo ni  soko la kimataifa
  • “Lengo la serikali ni kuona wafanyabiashara wanapata soko la madini ili waweze kuliingizia Taifa kipato,kulipa kodi halali na wao kunufaika kinaisha ma siyo kuzusha na kubambikiana mambo yasiyofaa ya uongo uongo”alisema Gambo.
BT
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa madini mara baada ya ufunguzi rasmi qa soko la madini mkoani Arusha.
  • Kwa upande wake Afisa madini mkazi Richard Robert mkoani Arusha akitoa taarifa amesema hadi sasa mkoa unakaribia kuwa na madini mbalimbalimbali kutokana na hali ya kijiolojia.
  • Amesema takwimu za madini mkoa wa Arusha kwa mwaka 2018-2019 zinaonyesha kuwa madini yenye thamani ya jumla ya shilingi 21,074,505,883.43,yaliuzwa na mrahaba ulipatikana zaidi ya shilingi764, 385,283.88 tzs,ambapo ada ya ukaguzi ni 208,653, 073.56,.
BT
Mkurugenzi wa AICC Elishilia Kaaya akitoa salamu kwa wafanyabiashara wa madini.
  • Amesema takwimu hizo zinadhihirisha kuwa mapato yanayokusanywa kutokana na madini 40% ya maduhuli yote,ambapo  hadi sasa mkoa wa Arusha umeshavuka lengo lililowekewa la kukusanya shilingi 2,500,000,000 kwa kiasi cha 102,419,194.95Tzs
BT
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wafanyabiashara na wa madini na wakazi wa Arusha kaika uzinduzi wa soko la Madini mkoani Hapo.
  • Umaarufu wa mkoa wa Arusha umejijenga zaidi miaka 30  iliyopita kwa kipindi cha  mwaka wa serikali 2018-19 Hadi sasa wapo wafanyabiashara 97 wafanyabiashara wadogo wa madini 291,ARUGEBA783 na TASGEDO 500.
  • Mkoa wa Arusha una ukubwa wa kilometa za mraba 37,576 una jumla ya leseni 784 za uchimbaji mdogo,leseni 4 za uchimbaji wa kati,leseni 42 za utafiti na leseni 1 ya uchenjuaji ambapo pamoja na utalii umekuwa kivutio cha biashara ya  madini
Ad

Unaweza kuangalia pia

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUKUA NA KUIMARIKA

Hali ya uchumi wa Tanzania yazidi kuimarika na kukua  kwa asilimia 6.9 ikiwa ni  takwimu …

Oni moja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *