KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO MHANDISI MTIGUMWE AMTEMBELEA MSINDIKAJI WA NAFAKA BUSEGA

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Tarehe 17 Juni 2019 akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu amepata fursa ya kumtembelea muwekezaji mzawa wa kusindika Nafaka Bw Deogratius Kumalija katika Wilaya ya Busega.
  • Akiwa kiwandani hapo Mhandisi Mtigumwe alipata maelezo kutoka kwa mmiliki huyo kuwa ameamua kujikita katika usindikaji wa mazao ya Nafaka kutokana na fursa iliyopo katika kuongeza thamani ya mazao hayo hususani mahindi na Mpunga.
MT
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Juni, 17 2019 akiwa mkoani Simiyu amepata fursa ya kumtembelea muwekezaji mzawa wa kusindika nafaka Bw. Deogratius Kumalija katika Wilaya ya Busega.
  • Bw Kumalija aliendelea kusema kuwa kiwanda hicho cha Mpunga kina uwezo wa kukoboa Tani 28 kwa siku na alisema kiwanda hicho kina uwezo wa kupanga madaraja ambapo kiwanda cha kusaga Mahindi kipo katika ujenzi na punde kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusaga tani zaidi ya 30 za mahindi kwa siku.
  • Alisema kuwa Viwanda Hivyo vitasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo na kuondokana na nchi kuendelea kuuza mazao ghafi.
MT
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe jana Juni, 17 2019 akiwa mkoani Simiyu amepata fursa ya kumtembelea muwekezaji mzawa wa kusindika nafaka Bw. Deogratius Kumalija katika Wilaya ya Busega.
  • Kadhalika, Mhandisi Mtigumwe alimpongeza muwekezaji huyo kuwa aendelee na uwekezaji huo pia Serikali imekuwa ikisisitiza kuyaongezea thamani mazao ya Kilimo.
  • Hivyo mwekezaji kama Bw Kumalija anatimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozw ana mHe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Sera ya Viwanda.
  • Hata hivyo kwa kuwa na Viwanda kama hivyo vitaongeza ajira na kuhamasisha wakulima kulima wakiwa na uhakika wa mazao yao na kuyaongezea thamani.Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 23 SKIMU YA UMWAGILIAJI NANGANGA WILAYANI RUANGWA KUWA IMEKAMILIKA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa siku 23 pekee kwa wakandarasi wanaojenga Skimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *