- Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hassunga jana tarehe 17 Juni, 2019 amefungua Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji kwenye sekta ya mbogamboga na matunda, jijini Mbeya katika ukumbi wa Hoteli ya Tughimbe, lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa shirikiana na Tanzania Horticulture Association(TAHA).
- Kongamano hilo la aina yale kufanyika Mkoa wa Mbeya, limehudhuriwa na washiriki 500 kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi.
- Wakizungumza katika kongamano hilo Viongozi walipata nafasi wameeleza kuwa wananchi wanapaswa kubadilisha mfumo wao wa kulima kimazoea na kulima kwa kulenga kilimo cha biashara.
- Aidha wamesema kuwa kilimo cha biashara kitakasidia kuleta mapinduzi chanya kwenye sekta ya kilimo ikiwemo kutengeneza ajira, kuongeza thamani malighafi katika sekta hiyo, kutosheleza mahitaji ya soko la nje, na kuwezesha wadau kujipatia kipato.
- Katika kufanikisha hilo, serikali imejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali hususan wa sekta biafsi ili kuondoa changamoto zinazokwamisha sekta ya kilimo kwa sasa ili kusaidia kukuza wawekezaji zaidi na kuzezesha sekta kukua katika asilimia/ kiwango kinachoridhisha.
- Fursa za uwekezaji zinazohimizwa kuchangamkiwa na wawekezaji katika sekta ya kilimo ni eneo lote la mnyororo wa uongezaji thamami sekta ya mbogamboga na matunda. Kongamano hili pia limehudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya jirani na Wilaya zake ndani ya Kanda za Nyanda za Juu kusini (Katavi, Songwe, Njombe, Rukwa na Ruvuma)
Ad