- Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki katika ofisi za Kiuo cha Uwekezaji (TIC). Ujumbe huo ulioongozwa na balozi wa Uturuki nchini Mheshimiwa Ali Davutaglu ulihusisha wafanyabiashara wa sekta za ujenzi, utalii, chakula na viwanda mbalimbali.
- Wafanyabiashara hao walielezea sifa ya Tanzania kuwa na amani kama kivutio cha wao kutaka kuwekeza nchini na kusema wangependa kufungua ofisi itakayokuwa kiungo baina ya wafanyabishara wa Uturuki na wale wa Tanzania.
- Mheshimiwa Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji akiahidi kuhakikisha Wizara ya Viwanda na Biashara ikishirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za Serikali itaharakisha taratibu zote zinazotakiwa ili waanze uwekezaji wao mapema iwezekanavyo. Pia aliahidi kuwakutanisha na wafanyabiashara wengine nchini ili wapate kufahamiana na kubadilishana ujuzi.
Ad