JAFO AAGIZA UJENZI WA HOSPITAL YA UHURU UANZE MARA MOJA

  • Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) ameagiza ujenzi wa Hospital ya Uhuru uanze Wiki ijayo Tar.24/06/2019 ili kutimizia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Dec, 2018 na kuelekeza fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
  • Waziri Jafo alitoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani Chamwino kukagua ujenzi wa hospital hiyo ya kisasa na  kukuta  hakuna ujenzi ulioanza na hata eneo  hilo halijasafishwa.
  • Akizungumza katika ziara hiyo Jafo amesema hataki kusikia hadithi zozote zinazokwamisha kuanza kwa ujenzi wa Hospital ya Uhuru kwa sababu Agizo lilishatoka na fedha zilishatengwa.
  • “Sikutarajia kukuta eneo la ujenzi likiwa katika hali hii, hakuna kitu kilichofanyika mpaka leo halafu mnaniambia bado mnaendelea na vikao sijui mnajadili nini ambacho hakiishi ninachotaka kuona hapa ni ujenzi kuanza mara moja yaani ikifika Jumatatu hali ya hapa iwe tofauti mkamilishe mambo yote yanayotakiwa kwa siku hizi chache na kazi hii ianze”
  • Waziri Jafo aliongeza kuwa nimesikia bado mnajadili kuhusu ramani gani itumike katika ujenzi huu sasa naagiza ujenzi wa Hospital hii utumie ramani ya Hospital ya Tunduma ambayo ni Gorofa kwa sababu ramani ile  itasaidia katika matumizi bora ya Ardhi na pia itakidhi mahitaji ya kuwa na jengo la kisasa lenye hadhi ya Hospital ya Uhuru.
  • Wakati huo huo Waziri Jafo aliagiza  kikosi maalumu cha SUMA JKT kitumike katika ujenzi wa hospital ya Uhuru ili iweze kwenda na muda na  ubora uweze kuzingatiwa na Wakala wa Majengo (TBA) watumike kama washauri na wadhibiti Ubora wa Majengo ya Hospital hiyo.
  • “Natoa miezi sita ujenzi wa Hospital hii uwe umekamilika na  ndio maana nikaagiza Kikosi cha Jeshi SUMAJKT  kitumike  ili tuweze kwenda na muda kwahiyo ifikapo Dec, 2019 nataka kuja kuona majengo yote  ya Hospiatl yakiwa yamekamika na kwa ubora wa hali ya juu” Alisema Jafo.
  • Akitaja sababu zilizochelewesha ujenzi wa Hospital ya Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belnith Mahenge amesem  michoro ya Hospital imechelewa kupatikana na zaidi fedha zilizoelekezwa hazijaingia kwenye Akaunti husika ili ziweze kutumika kwenye  ujenzi.
  • Aidha Rc Mahenge  alimshkuru Waziri Jafo kwa ziara yake na kusema maagizo yote yaliyotolewa yamepokelewa  na yatatekelezwa; Ujenzi wa Hospital ya Uhuru  utaanza mara moja.
  • Ujenzi wa Hospital ya Uhuru ni Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa mwezi Dec, 2018 ambapo aliagiza shilingi bil. 900  zilizokuwa zitumike kwenye  sherehe za maadhimisho ya Uhuru  wa Tanzania zitumike kujenga Hospital Kisasa Mkoani Dodoma na  kuongezafedha zaidi shilingi  Bil 2.5 kutoka katika Gawiwo lililotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel.Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

2 Maoni

  1. I was looking at some of your blog posts on this internet site and I
    believe this internet site is real informative!
    Keep putting up.!

  2. This is a really good tip especially to those fresh to the blogosphere. Short but very precise information… Thank you for sharing this one. A must read article!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *