SERIKALI YAJIPANGA KUTEKA SOKO LA WATALII CHINA

  • Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwa sasa muelekeo wa soko la Utalii nchini umelenga kupata watalii wengi kutoka nchini China na kama Wizara inayoshugulikia masuala ya Utalii,  suala la  kujifunza lugha ya kichina kwa baadhi ya watumishi na wadau wa utalii ili kuteka soko hilo ni jambo lisiloepukika.
UT
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza jambo na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS mara baada ya kuwatambulisha wageni hao Bungeni Dodoma leo waliokuja nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa mafunzo watumishi na wadau wa utalii nchini
  • Imesema nguvu nyingi kwa sasa zinaelekezwa nchini China hivyo  ni muda muafaka wa kuandaa timu ya wataalamu mbalimbali wakiwemo  waongoza watalii watakaoweza kuzungumza lugha ya kichina ili kuweza kulimudu soko hilo.
  • Hayo yamesemwa leo  jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu  wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi wa  Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii  cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS
UT
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhiwa zawadi ya pichana Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa mafunzo ya chuo hicho ,Wanga Jiaxin leo katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
  • Amesema  lengo mkutano huo ni  kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania katika suala la kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa Utalii nchini.
UT
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akikabidhiwa zawadi ya pichana Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa mafunzo ya chuo hicho ,Wanga Jiaxin leo katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
  • Mkutano huo  umehudhuriwa na ujumbe kutoka China ukiongozwa na Makamu wa Chuo hicho,Prof.Xiong Nanyong,Kaimu huku kwa upande wa Wizara  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Lucius Mwenda pamoja na ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.
UT
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi ya vitabu kutoka TANAPA ikiwa ni ishara ya shukrani kwa Mkuu wa kitengo cha mafunzo wa chuo cha JXCFFS, Yang Jing mara baada kufanyika mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano katika ya China na Tanzania jijini Dodoma.
  • Amesema ni muhimu kwa watumishi wa wizara pamoja na wadau wa utalii kujiandaa ili kuweza kuzungumza lugha ya kichina badala ya vifaa maalum vya kutafsiri lugha ilhali kuna uwezekano kwa Watanzania kujifunza.
UT 5-01
Naibu wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS mara baada ya kumaliza mkutano uliolenga kumaimarisha mahusiano baina ya Tanzania na China.
  • Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Xiong Nanyong amesema wamejipanga kutoa mafunzo mbalimbali likiwemo suala la lugha ya kichina pamoja na utalii ili kuwajengea uwezo Watumishi hao
UT
Makamu wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS Prof.Xiong Nanyong ( wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya picha ya Chuo hicho Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bw. Lucius Mwenda mara baada ya kufanyika mkutano mara baada kufanyika mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano katika ya China na Tanzania jijini Dodoma.
  • Ameongeza kuwa tayari wameshaomba kibali kutoka Ofisi ya Rais Utumishi wa umma na Utawala Bora  kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo nchini.
UT
Viongozi wa Chuo cha Mafunzo ya kigeni na Utalii cha nchini China kijulikanacho kwa jina la JXCFFS wakiwa wamesimama wakati wakitambulishwa Bungeni jijini Dodoma
  • Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lucius Mwenda  ameahidi kutoa ushirikiano kwa Uongozi wa Chuo hicho ili  kujengeana uwezo  baina ya Serikali ya  Tanzania na China.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *