- Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa yupo ziarani katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es salaam ili kujionea mwenendo wa hali ya ubora wa zao la korosho kwenye maghala.
- Mhe Bashungwa amesema kuwa kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi katika maeneo mengi kuhusu ubora wa korosho kuwa mbovu jambo ambalo halina ukweli. “Nilikuwa nikisikia na kutumiwa ujumbe na watu mbalimbali kuwa korosho zilizonunuliwa na Serikali ni mbovu hivyo nimelazimika kufunga safari ili kutembelea maghala ambayo yamehifadhi korosho ili kubaini ukweli uliopo.
- Jambo muhimu kwa sasa tunatafuta masoko kwa ajili ya kuziuza korosho zote” Alikaririwa Mhe Bashungwa. Alisema kuwa, hali ya ubora wa korosho ilisababishwa na habari za uongo zilizopo mitaani kuwa hazina ubora. Kwa maghala niliyopita kujionea na hali ya korosho ipo katika hali nzuri.
- Aidha, Waziri huyo wa viwanda na Biashara amewasihi wafanyabiashara mbalimbali kujitokeza kuchangamkia fursa ya ununuzi wa korosho hizo.(Mathias Canal)
Ad