Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.

WAZIRI BASHUNGWA AWATOA HOFU WAFANYABIASHARA KUHUSU UBORA WA KOROSHO

KS 1-01
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akikagua korosho
KS
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akiwa
  • Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa yupo ziarani katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Dar es salaam ili kujionea mwenendo wa hali ya ubora wa zao la korosho kwenye maghala.
  • Mhe Bashungwa amesema kuwa kumekuwa na dhana potofu kwa wananchi katika maeneo mengi kuhusu ubora wa korosho kuwa mbovu jambo ambalo halina ukweli. “Nilikuwa nikisikia na kutumiwa ujumbe na watu mbalimbali kuwa korosho zilizonunuliwa na Serikali ni mbovu hivyo nimelazimika kufunga safari ili kutembelea maghala ambayo yamehifadhi korosho ili kubaini ukweli uliopo.
  • Jambo muhimu kwa sasa tunatafuta masoko kwa ajili ya kuziuza korosho zote” Alikaririwa Mhe Bashungwa. Alisema kuwa, hali ya ubora wa korosho ilisababishwa na habari za uongo zilizopo mitaani kuwa hazina ubora. Kwa maghala niliyopita kujionea na hali ya korosho ipo katika hali nzuri.
  • Aidha, Waziri huyo wa viwanda na Biashara amewasihi wafanyabiashara mbalimbali kujitokeza kuchangamkia fursa ya ununuzi wa korosho hizo.(Mathias Canal)
Ad

Unaweza kuangalia pia

KILA MTANZANIA ANAWEZA KUWEKEZA, TUMIENI FURSA ZILIZOPO – WAZIRI KAIRUKI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *