- Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya ziara wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu kuwezesha wananchi wote wanaopitiwa na miradi ya umeme vijijini (REA), kulipia shilingi 27,000 tu bila kujali ni vijijini au katika Halmashauri za Wilaya.
- Alifanya ziara hiyo jana, Juni 20, 2019 ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika Taasisi mbalimbali za Umma zikiwemo Shule na Zahanati.
- Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Bicha, Kolo na Kwayondu, Naibu Waziri alimpongeza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wilayani humo, Emily Ntanzimila, kutokana na kutekeleza kwa haraka agizo hilo lilitolewa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati.
- “Hongera sana maana nimeona hapa kwenye orodha majina ya wananchi ikiambatishwa na risiti za malipo waliyofanya ambazo zinasomeka wamelipia shilingi 27,000 tu kama tulivyoelekeza.”
- Akifafanua kuhusu agizo hilo la Serikali, Naibu Waziri alisema kuwa, awali, gharama iliyokuwa ikitozwa ilikuwa inatofautiana kwani miradi ya REA ilikuwa shilingi 27,000 lakini ilipokamilika na kukabidhiwa kwa TANESCO, wateja walilazimika kuunganishiwa umeme kwa shilingi 177,000.
- “Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kutoa maelekezo kwamba, umeme unaletwa kwa ajili ya kutumiwa na wananchi, hivyo bei iwe moja tu yaani shilingi 27,000.”
- Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika eneo lake, Meneja wa TANESCO Kondoa, alimweleza Naibu Waziri kuwa vijiji vyenye umeme wilayani humo ni 29 kati ya 84 vilivyopo, ambavyo ni sawa na asilimia 34.
- Alisema, kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu ambayo inaendelea kutekelezwa, vijiji vingine 23 vinatarajiwa kuunganishwa hivyo kufikia 52, sawa na asilimia 62.

- Aliongeza kuwa, asilimia 38 ya vijiji vilivyobaki (vijiji 32), vimependekezwa kwenye miradi ya REA ya Ujazilizi, REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kwenye Bajeti ya TANESCO mwaka 2019/2020.
- Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alimwagiza Meneja huyo kufika eneo la Itundwi wilayani humo siku ya Jumatatu, Juni 24, mwaka huu, ili apokee malipo ya umeme ya wananchi ambao awali aliwarudisha.
- Naibu Waziri alitoa maagizo hayo baada ya wananchi wa eneo husika kusimamisha msafara wake na kutoa malalamiko kadhaa ikiwemo hilo la kukataliwa kupokelewa malipo yao ya kuunganishiwa umeme.
- “Tumeshatoa maelekezo kwa Mameneja wote wa TANESCO nchi nzima kuwa ni marufuku kukataa kupokea malipo ya umeme kutoka kwa wananchi kwa kisingizio chochote kile. Naamini wakati akiwarudisha tulikuwa bado hatujatoa maelekezo, hivyo namwagiza arudi kupokea malipo yenu.”
- Aidha, alimtaka Meneja huyo kufanyia kazi utaratibu wa kuwaunganishia umeme wananchi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na miundombinu lakini hawana nishati hiyo, kupitia Mradi wa Ujazilizi.
- Katika ziara hiyo, Naibu Waziri alifuatana na viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu kutoka wizarani, TANESCO na REA.Na Veronica Simba – Dodoma
Ad