RAIS MAGUFULI AWAPONGEZA WANANCHI WA CHATO KWA KUCHAPA KAZI NA KUJILETEA MAENDELEO

MG 3-01

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza wananchi wa Chato Mkoani Geita kwa kuitikia wito wa Serikali wa kuongeza juhudi katika kazi za uzalishaji mali hali iliyoiwezesha Wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
MG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita baada ya kuwasili mkoani humo kwa mapumziko
  • Mhe. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo tarehe 01 Julai, 2019 wakati akiwasalimu wananchi hao katika eneo la Njiapanda, muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Chato akitokea Jijini Dar es Salaam.
MG 7-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita baada ya kuwasili mkoani humo kwa mapumziko
  • Amefafanua kuwa akiwa angani kabla ya kutua amefurahishwa kuona jinsi wananchi wa Chato walivyochangamka kimaendeleo kwa kujenga nyumba za kuishi za kisasa, majengo ya biashara, majengo ya huduma za jamii na mashamba ya mazao mbalimbali.
MG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita baada ya kuwasili mkoani humo kwa mapumziko
  • “Nawapongeza sana wananchi wa Chato, mnachapa kazi kwelikweli na maendeleo yanaonekana, Chato inabadilika. Nilishasema asiyefanya kazi na asile, kwa hiyo tuendelee kushikamana kufanya kazi na kujenga nchi yetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
MG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika ndege katika  uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita baada ya kuwasili mkoani humo kwa mapumziko
  • Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kushikamana na kutobaguana ili kwa pamoja waijenge Tanzania ambayo ina rasilimali nyingi.
  • Kabla ya kuwasalimu wananchi wa Njiapanda, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu na kuwashukuru wananchi wanaofanya kazi za ujenzi katika uwanja wa ndege wa Chato.
  • Mhe. Rais Magufuli amewasili leo katika Kijiji cha Mlimani Wilayani Chato kwa Mapumziko.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *