MKUCHIKA: TANZANIA INAZIDI KUPATA HESHIMA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

  • Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), George Mkuchika amesema Tanzania inaendelea kupata heshima kubwa katika Jumuiya ya Kimataifa katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa kutokana na mshikamano na nguvu ya pamoja iliyopo katika vyombo na taasisi zinazosimamia utawala bora nchini.
  • Akizungumza katika kongamano la siku maalum dhidi ya rushwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam leo Jumatano (Julai 3, 2019) Waziri Mkuchika alisema utafiti uliofanywa na taasisi hizo zimesifu juhudi za zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya mfano katika vita vya mapambano dhidi ya rushwa.
MK
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifurahia jambo katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
  • Mkuchika aliasema taasisi hizo zikiwemo MO Ibrahim, Transparency International, APRM na taasisi nyingine kubwa duniani zinazosimamia masuala ya utawala bora zimefanya utafiti na kusifu juhudi kubwa zinazofanywa na  serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo tafiti mbalimbali zimeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili nyuma ya nchi ya Rwanda.
  • Waziri Mkuchika alisema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kuweka mkazo na msukumo  katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo taasisi zote zinazosimamia masuala ya utawala bora zimekuwa zikiunganisha nguvu ya pamoja na kulifanya suala la rushwa sasa kuwa na nguvu na msukumo mpya wa mapambano katika jamii.
MK
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifurahia jambo katika kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally.
  • “Kwa sasa vyombo vyetu vyote serikalini si TAKUKURU pekee bali pia polisi, tiss (usalama wa taifa), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ICAG) na vingine vyote, vimeendelea kuunga katika kusimamia masuala ya utawala bora na hili limeleta msukumo na hamasa mpya katika vita dhidi ya rushwa hapa nchini” alisema Waziri Mkuchika
  • Akizungumzia rushwa katika sekta ya viwanda na biashara, Waziri Mkuchika alisema Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali katika kupunguza tatizo hilo ambalo limekuwa likiathiri sekta binafsi ambayo imekuwa mshirika wa karibu wa serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
MK
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally, akiteta Jambo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Musa Assad, kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius NyerereJijini Dar es Salaam,
  • Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika alisema rushwa katika sekta biashara imekuwa ikiathiri sana masuala ya uwekezaji wa kigeni, ambapo eneo lililonyesha kutawala kwa rushwa ni katika eneo la utoaji wa vibali na leseni kutoka katika taasisi na idara muhimu za serikalini na hivyo serikali imeendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa kwa wawekezaji na hivyo kuharakisha ukuaji wa uchumi.
  • Akifafanua zaidi Mkuchika anasema kutokana na serikali kutambua mchango wa sekta ya viwanda na biashara katika kukuza uchumi na uzalishaji wa ajira nchini ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali imekuwa ikifanya marekebisho mbalimbali ya sheria na sera mbalimbali ambazo zimekuwa ni sehemu ya mianya ya rushwa nchini ikiwemo eneo la kodi.
MK 5-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akifuatilia mada mbalimbali kwenye kongamano la siku maalum dhidi ya Rushwa iliyofanyika katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dkt.Bashiru Ally na kulia ni Mkurugenzi Mkuu Takukuru, Diwani Athuman.
  • “Kutokana na kudhibiti rushwa kwa sasa kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya mwezi yameweza kuongezeka kutoka Tsh Bilioni 800 kwa mwezi hadi kufikia Tsh trilioni 1.3 hii inaoyesha kuwa kulikuwa na maeneo ambayo kulikuwa na uvujaji wa mapato ya serikali kulikochangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo rushwa”
  • Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athumani alisema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi kupitia Mpango Mkakati dhidi ya mapambano ya rushwa (NASCAP III) ili kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya rushwa yanapata mafanikio nchini.
  • Anaongeza kuwa kupitia NASCAP III, ofisi yake imeendelea kutekeleza masuala mbalimbaliu ikiwemo kufanya tafiti kubaini ukubwa na kiwango cha rushwa nchini, kupokea maoni, kutoa elimu kwa umma kupitia makongamano, rushwa pamoja na kufanya uchunguzi na kufungua mashtaka kwa watu mbalimbali wanaopatikana na hatia dhidi ya rushwa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI INATEKELEZA MPANGO KAZI WA BLUE PRINT ILI KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI

Wadau wote kupitia vyama vyao waitwa kuleta mapendekezo ili kuboresha sekta zao ikiwa Serikali ipo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *