MKURUGENZI MKUU WA OFISI YA TAKWIMU AKUTANA NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA

  • Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho amesema Serikali ya Nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takiwmu (NBS) kwa ajili ya kuimarisha miundombinu yake ikiwemo mifumo ya Tekonojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kumalizia Ujenzi wa Ofisi za NBS katika Mikoa ya Dodoma na Kigoma.
TK 1-01
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Balozi wa Jamhuri ya Korea Nchini, Tae-ick Cho (katikati) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika leo (Ijumaa Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtaalamu wa Utafiti wa Ubalozi wa Korea, Hae-ju Yong
  • Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa leo Ijumaa (Julai 5, 2019) Jijini Dar es Salaam, Balozi Cho amesema Serikali yake ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika katika kuhakikisha kuwa NBS inatekeleza majukumu yake.
TK
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa yaliyofanyika leo Ijumaa Julai 5, 2019 katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Takwimu za Kilimo wa NBS, Titus Mwisummba na Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Bw. Daniel Masolwa.
  • Balozi Cho alisema Serikali ya Jamhuri ya Korea inatambua umuhimu wa takwimu katika shughuli za kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, hivyo itahakikisha kuwa mahitaji yote ya msingi kwa yanayohitajika na NBS ikiwemo uimarishaji wa miundmbinu ya TEHAMA inapewa kipaumbele.
TK 3-01
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho akimwonesha nakala ya jarida Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa kuhusu miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelzwa na Serikali ya Nchi hiyo Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa NBS, Bw. Daniel Masolwa. Mkutamo baina ya Balozi huyo na NBS ulifanyika leo Ijumaa (Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam.
  • Aidha Balozi Cho aliongeza kuwa Serikali ya Korea itahakikisha kuwa makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa kwa haraka kwa kuwa inatambua ukubwa na umuhimu wa majukumu ya NBS katika uzalishaji na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kuharakisha shughuli za Maendeleo ya wananchi.
TK 4-01
Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) na baadhi ya watendaji wa NBS akiwemo Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi- Daniel Masolwa kulia, mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao leo (Ijumaa Julai 5, 2019) katika Ofisi za NBS Jijini Dar es Salaam.
  • Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa alisema NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tayari ilianza hatua za awali za makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Korea na hivyo kupitia sheria ya misaada ambapo wameahidi kujenga na kuimarisha miundombinu ya Ofisi za NBS zilizopo katika Mikoa ya Kigoma na Dodoma.
  • “Katika Mkoa wa Kigoma wameahidi kujenga Ofisi hiyo na kusimika miundombinu ya TEHAMA wakati katika Mkoa wa Dodoma wameahidi kuweka miundombinu ya TEHAMA katika Jengo la Ofisi zetu za Dodoma” alisema Chuwa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAKAZI WA PEMBEZONI MWA BAHARI WAELIMISHWA ATHARI ZA MAGENDO

Wakazi na wafanyabiashara waishio pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi katika kata za Somangila, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *