ALIYELAZWA MWAKA MMOJA MLOGANZILA APATIWA MASHINE YA KUPUMUA

  • Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, imempatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad Awadhi kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yanamlazimu kutumia mashine ya oxygen muda wote ili aweze kupumua.
ML 5-01
Bw. Hamadi Awadhi akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Muhimbili-Mloganzila kwa huduma aliyoipata na kwa kumpatia msaada ambao utamuwezesha kuendelea na shughuli zake za kawaida.
  • Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-Prof. Charles Majinge amesema hospitali imempatia msaada Bw. Awadhi kwa lengo la kuokoa maisha yake sanjari na kuimarisha afya yake lakini pia kumuwezesha kuendelea na shughuli zake za kawaida ili kutokua tegemezi kutokana na hali yake.
  • Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru ameeleza kwamba mashine hiyo inathamani ya shilingi milioni tatu na nusu imenunuliwa na Hospitali ya Mloganzila ambapo wataalam wamempatia mafunzo Bw. Awadhi namna ya kuitumia na kuitunza ipasavyo.
ML 4-01
Dkt. Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri (kulia) akizungumzia kuhusu matibabu aliyopatiwa Bw. Awadhi kwa kipindi chote alichokua amelazwa hospitalini
  • Prof. Museru amemtaka Bwan. Awadhi kuitunza na kuitumia vema mashine hiyo kama ambavyo ameelekezwa na wataalam ili afya yake itakapoimarika iweze kusaidia watanzania wengine.
ML 3-01
Prof. Lawrence Museru (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MNH Prof. Majinge (wa pili kuli) kuhusu ununuzi wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) ambayo imegharimu shilingi milioni tatu na nusu, kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi.
  • “Hospitali imekupatia msaada wa mashine hii ya kukusaidia kupumua- kwa lengo la kuhakikisha afya yako inaimarika zaidi hivyo tunaomba uitunze na utakapopona kabisa utairejesha hospitali ilituwasaidie wengine” amesema Prof. Museru.

ML 1-01

  • Naye Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri amesema, Bw. Awadhi kwa muda wote aliokuwepo hospitalini ameishi kwa kutegemea mashine ya oxygen ambayo inamsaidia kupumua ambapo kwa siku alikua akitumia gesi wastani wa lita 5,760.
  • Bw. Hamad Awadhi alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Julai 9 mwaka 2018 na kuruhusiwa Julai 9 mwaka 2019 baada ya afya yake kuimarika.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *