MHANDISI KAKOKO: NCHI ZA SADC ZIIMARISHE NGUVU YA PAMOJA YA MIUNDOMBINU KUKUZA VIWANDA

  • Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuimarisha miundombinu ya Reli, Barabara, Bandari pamoja na Mawasiliano ili kukuza sekta ya viwanda katika Mataifa hayo.
KK 2-01
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi, Dotto James akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo kwa wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi nchini mara baada mafunzo yao leo Jumapili (Agosti 4, 2019) Jijini Dar es Salaam. . Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa na kulia kwa Mgeni rasmi ni Mkurugenzi Msaidizi- idara ya Ajira na Ukuzaji ujuzi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Ahmed Makbel.
  • Aliyasema hayo leo Jumanne (Agosti 6, 2019) wakati wa mjadala wa wataalamu uliojadili umuhimu  ya sekta ya miundombinu katika  ujenzi wa uchumi wa Viwanda katika Nchi Wananchama wa SADC,  katika Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

KK 3-01

  • Mhandisi Kakoko alisema kwa sasa Tanzania imekuwa nchi ya mfano katika nchi za Ukanda huo, kwa kuwa imekuwa kitovu cha usafirishaji wa bidhaa na malighafi mbalimbali katika nchi za SADC, hatua iliyotokana na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuimarisha Bandari, Reli na mtandao wa barabara.
  • “Zipo Nchi chache ndani ya SADC ikiwemo Afrika Kusini ambazo tayari zimepata mafanikio makubwa katika miundombinu yake ikiwemo Bandari ya Durban, hivyo mkutano huu unakuwa chachu kwa Mataifa yote kuweza kubaini changamoto zilizopo ili kuhakikisha tunakuwa na mkakati wa pamoja wa kutuvusha hapatulipo” alisema Kakoko.

KK 4-01

  • Aliongeza kuwa ili kufikia mafanikio hayo Serikali za SADC hazina budi kuweka msisitizo katika kuziwezesha sekta binafsi ikiwemo mashirika ya maendeleo ya kimataifa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya miundiombinu pasipo na kuweka masharti magumu kwa serikali, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuleta manufaa kwa wananchi walio wengi.

KK 5-01

  • Kwa mujibu wa Kakoko alisema Serikali kupitia TPA imeanza kuchukua hatua mbalimbali katika kuimarisha kiwango cha ushindani na Bandari nyingine kubwa Barani Afrika na hivyo kuweza kukuza uchumi wa Nchi pamoja na kuwa kichocheo muhimu katika maisha ya wananchi.

KK 6-01

  • Aidha Kakoko alisema miundombinu ya Nchi za SADC kwa sasa si mizuri kwa kuwa zimekuwa zikitumia gharama kubwa za fedha kwa ajili ya kugharamia miundombinu  hivyo ni  wajibu wa Mashirika na Taasisi za umma na binafsi kujitokeza ili kusaidia uboreshaji na ujenzi wa miundombinu hiyo na hivyo kurahisisha uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI SADC, BALOZI WA EU NA BALOZI WA CHINA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Februari, 2020 amekutana na Katibu Mtendaji wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.