MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI AIPONGEZA SERIKALI KWA KUJENGA RELI YA KISASA KWA FEDHA ZAKE ZA NDANI

  • Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe amefanya ziara fupi kuona Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Agosti 22, 2019.
RL 1-01
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akisiliza maelezo kutoka kwa wataalam wanaojenga reli ya kisasa
  • Katika ziara hiyo Bi. Anne alipata fursa ya kutembelea Stesheni ya reli ya kisasa inayojengwa eneo la Stesheni jijini Dar es salaam pamoja na kutembelea eneo la Vingunguti kuona kipande cha reli ya kisasa kilichotandikwa eneo hilo ambapo Bi Anne alionesha kufurashishwa na kasi ya ujenzi.
  • “Nimekuja kuona hatua kubwa ambayo serikali imechukua ya kujenga reli ya kisasa ninachoweza kusema kwa niaba ya nchi ninazoziwakilisha ni kwamba huu si mradi wa Tanzania pekee bali ni mradi wenye manufaa kwa nchi zilizofungamana katika ukanda huu” alisema Bi. Anne
  • Aidha Bi. Anne ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kwa kutumia mapato ya ndani pia ameahidi kuwa Balozi kueleza yale aliyoyaona katika Mradi wa SGR
RL 2-01
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akisiliza maelezo kutoka kwa wataalam wanaojenga reli ya kisasa
  • “Naipongeza serikali ya Tanzania kwa kuamua kujenga mradi huu kwa kutumia vyanzo vya ndani” Nitafikisha ujumbe huu juu ya hiki tulichokiona leo” alisema Bi. Anne
  • Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa taasisi za kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia zinaweza kukamilisha Mradi huu kwa kuufadhili siku zijazo
  • “Ni matumaini yangu kwamba kwa siku zijazo tutakapokuwa tunatafuta njia za kufadhili mradi huu taasisi za kimataifa ikiwemo benki ya dunia tutaweza kuja kukamilisha mradi huu” alisema Bi. Anne
  • Naye Kaimu Mkurugenzi wa Ujenzi na Miundombinu ya Reli Mhandisi Felix Nlalio amesema kuwa wameupokea ujio huo kwa furaha na kwa kuwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia amejionea mwenyewe kasi ya ujenzi na amefurahishwa na ubora wa wa kazi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI INATARAJIA KUJENGA MINARA 5 YA MAWASILIANO WILAYANI MAFIA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Atashasta Nditiye (Mb.) amezindua mnara wa Mawasiliano …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *