- Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji kuwa na tekinolojia mpya na ya uhakika ili kufanikisha mkakati wa Seikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wa kukuza uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2015 kupitia sekta ya viwanda.
- Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 28, 2019) katika Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on African Development (TCAD 7) uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye ukumbi wa hoteli ya Pacifico Yokohama nchini Japan.
- Waziri Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo amesema kwamba ujenzi na uendeshaji wa uchumi wa viwanda unahitaji sana teknolojia kutoka ndani na nje ya nchi.
- Amesema ujezi wa uchumi wa viwanda utajikita katika matumizi ya malighafi yanayopatikana nchini kama vile mazao ya kilimo, uvuvi, mifugo na madini kwani Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo pamoja na kuwa mali asili nyingi.
- Waziri Mkuu amesema hivi sasa Tanzania inaandaa miundombinu na huduma mbalimbali zitakazofanya uwekezaji katika sekta ya viwanda ufanyike katika mazingira yanayokidhi matarajio ya wawekezaji na wateja wao.
- Ametoa mifano wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere katika mto Rufiji, ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR , ujenzi wa barabara za lami, ufufuaji wa Shirika la Ndege la Tanzania na upanuzi wa Bandari za Dar es salaam, Mtwara na Tanga kuwa ni baadhi ya mipango ya Serikali ya kuifanya nchi iwe na sifa na viwango katika suala la uwekezaji wa viwanda.
- “Utaratibu wa Blue Print ulioandaliwa na Serikali kwa lengo la kuondoa kero mbalimbali katika uwekezaji na biashara nchini Tanzania ni mfano hai unaodhihirisha kamba Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kushirikiana na sekta binafsi kujenga uchumi wa viwanda.”
- Awali,akifungua mkutano huo, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, uwekezaja uliofanywa Barani Afrika na wawekezaji binafsi kutoka nchini Japan umefikia Dola za Marekani bilioni 20. Ameahidi kuwa uwekezaji huo utaendelea kuengezeka.
- Viongozi mbali mbali kutoa nchi za Afrika wamehudhuria mkutano huo akiwemo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Uganda, Yoweri Musseveni pamoja na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravini Kumar.
- Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ad
I like this website very much, Its a real nice billet to read and receive information.Raise range