NEEMA YA GESI ASILIA YANUKIA MIKOANI

  • Wizara ya Nishati (Tanzania) na Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Oktoba 17, 2019 walikutana katika ofisi za  Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma na kujadili Mkakati wa kufikisha gesi asilia katika mikoa mbalimbali nchini.
  • Kikao hicho, kilichoongozwa na Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi, kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara, Haji Janabi na maafisa kutoka wizarani na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC.)
  • Katika kikao hicho, JICA waliwasilisha rasimu ya Mkakati tajwa waliouandaa kwa kushirikiana na watalaamu wa Wizara na TPDC.
  • Mkakati huo umeainisha mahitaji ya nishati kwa mikoa mbalimbali nchini na kupendekeza namna bora ya kufikisha gesi katika mikoa hiyo kulingana na mahitaji.
  • Aidha, mkakati huo umejumuisha uchambuzi wa kiuchumi kwa kila njia pendekezwa ili kuona ni ipi itakuwa na manufaa zaidi. Njia zilizopendekezwa ni kupeleka gesi kwa njia ya mabomba, gesi iliyogeuzwa kimiminika au gesi iliyogandamizwa.
  • Wizara kupitia TPDC inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kusmbaza gesi asilia na kuunga wateja katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Mtwara kwa kuanzia.
  • Kukamilika kwa Mkakati wa kufikisha gesi katika mikoa mingine na kuanza kwa utekelezaji wake, kutawezesha wananchi wengi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini kutumia gesi asilia ambayo ni nafuu na rafiki kwa mazingira ikilinganishwa na vyanzo vingine vya nishati.
  • Ujumbe wa JICA uliongozwa na Kenekiyo Kenekiyo, Mshauri katika Taasisi ya Masuala ya Nishati Japani (IEEJ)
Ad

Unaweza kuangalia pia

TPDC YAOKOA TRILIONI 12.7 KUAGIZA MAFUTA NJE YA NCHI

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *