WAZIRI JAFO AZITAKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUWATUMIA IPASAVYO WATAALAM SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo ameagiza Wizara yake kuhakikisha wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii wanapewa jukumu la kusimamia kazi  ya  Bima ya Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri kwa kuwa ndio wenye utaalam wa kuhamasisha jamii.
  • Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii lililofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu nakuwataka wataalam hao kutumia taaluma yao iposavyo kufanikisha zoezi hilo.
14-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo pamoja na mke wakeamabye pia ni Afisa Maendeeo ya Jmaii mkoa wa Dodoma wakifurahia zawadi iliyotolewa na wataalam wa maendeleo ya jamii mara baada ya waziri huyo kufunga kongamano lao.
  • Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa kazi hiyo imekuwa ikitekelezwa na wataalam wa sekta ya Afya ambao kitaaluma wana fani ya tiba na madawa lakini linapokuja suala la uhamasishaji wa jamii kuhamasika kushiriki masuala ya maendeleo ni wataalam wa maendeleo ya jamii waliobobea katika fani hiyo.
  • “Katika wafanyakazi ambao wamekuwa hawapewi kipaumbele na kudhalauliwa katika maeneo yao ya kazi ni wataalam wa maendeleo ya jamii lakini sasa wakati umefika kuwapatia vitendea kazi na kuwatumia katika shughuli zote za maendeleo ya Taifa”. Aliongeza Waziri Jaffo.
13-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo akikabidhiwa zawadi na Rais wa Chama cha Maafisa Maendeleo ya Jamii CODEPATA Bw. Wambura Sunday huku viongozi wengine wa Wizara yenye dhamana na Maendeleo ya Jamii wakishuhudia mara baada ya kufunga kongamano la wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
  • Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa kwa kipindi kirefu wataalam hawa wamekuwa hawatumiki ipasavyo na badala yake wamekuwa wakitumiwa wakati wa dharula au katika kazi za zimamoto wakati ukiangalia watumishi wengi wa serikali wataalam hawa ni moja ya kada yenye wasomi wengi.
  • Kufuatia ari hiyo waziri Jafo ameagiza mamlaka zilizochini ya Serikali za mitaa Nchini kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ya wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii kwa kuwapatia vitendea kazi ikiwemo kuhakikisha wanapatiwa magari ili waweze kufuatilia kazi zao vizuri tofauti na sasa ambapo mazingira yao ya kazi yana hali duni.
12-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakiimba wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii lilofanyika jijini Dodoma.
  • Waziri Jafo pia amewataka wataalam hao wa maendeleo ya jamii kujiamini katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanasimamia misimamo katika vikao vya mbalimbali vya maamuzi ikiwemo CMT ili waweze kukubalika na kuaminika kama ilivyo kada nyingine katika maeneo yao ya kazi.
  • Waziri huyo amewaagiza watendaji kazi wote serikalini kufanya kazi kwa bidii ili hata mtumishi akienda likizo wanaobaki ofisini waone umuhimu wake lakini kama mtumishi akiama au kwenda likizo na watu wasione upungufu wowote ujue mtumishi huyo hatoshi katika eneo hilo.
11-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Serikali Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo akiongea wakati wa kufunga Kongamano la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii lilofanyika jijini Dodoma.
  • Wakati huohuo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu katika salamu zake kwa waziri huyo alisema kuwa kongamano la wataalam wa maendeleo wa jamii limekuwa na mada ambazo kimsingi zitawaletea mabadiliko katika utendaji kazi wao ikiwemo mada ya kuamsha ari ya wananchi kuoresha makazi yao.
  • Aidha Dkt Jingu amesema kongamano hilo limekuja na maadhimio na mapendekezo yanayoangazia namna bora ya utendaji kazi wao lakini kutokana na kongamano hilo wataalam hawa wamejiwekea malengo yanayopimika kwa mstakabali wa taaluma yao.
  • Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKATIBU WAKUU SMT NA SMZ WAKUTANA ZANZIBAR

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *