- Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula leo amefungua Mkutano wa Makatibu Wakuu wa afya wa nchin wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amesema mkutano huo utapitia ajenda kuu 13 za mkutano zitakazojadiliwa kwenye mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC.
- Akizungumza Dkt Chaula amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kukabiliana na Kifua Kikuu ambapo Vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimepungua kutoka 9.6% mwaka 2015 mpaka kufikia 4.6% mwaka 2018.
- Aidha amesema kwa upande wa Malaria Tanzania imeongeza kiwango cha upimaji kutoka 64% mwaka 2015 mpaka 99% mwaka 2018, maambukizi yamepungua kwa 67% kutoka watu 164 kwa kila watu 1000 hadi watu 119 kati ya 1000 na vifo vimepungua kwa 63% kutoka 6737 hadi 2540”. Dkt. Chaula
- “Kwa upande wa maambukizi ya VVU, Tanzania imepunguza maambukizi kwa watu wazima kwa asilimia 20.6 na asilimia 31.3 kwa watoto walio chini ya miaka 15 katika kipindi cha mwaka 2010 na 2018”. Dkt. Chaula.
- Dkt. Chaula amesema Serikali ya inaedelea kupambana na tatizo la udumavu kwa watoto wadogo kwa kutoa huduma katika maeneo yaliyoathirika, mpaka kufikia mwaka 2018 tatizo hilo limepungua kutoka 34.4% mwaka 2015 hadi kufikia 31.8% mwaka 2018
- Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa sekta ya Afya na Ukimwi unafanyika jijini Dar es salaam na utamalizika Novemba 8, 2019
Ad