“Jukumu lililochukuliwa na Julius Nyerere na Kenneth Kaunda halipaswi kupuuzwa. Nyerere alikuwa maarufu sana katika nchi za Scandinavia. Na alikuwa anazungumza wazi pale lilipohusu Kusini mwa Afrika, na kila wakati alikuwa akizungumza, wakati alipotembelea Norway, nchi yake haikujiona huru kama Afrika Kusini haikuwa huru. Na Kaunda, ambaye pia alikuwa akiheshimiwa sana nchini Norway, alisimama kidete, na alijitolea kwa uzito sana. Na ingawa ukweli ni kwamba msaada toka kwa wanorwey ulipitia Zambia na Tanzania haikuwa tu kwa bahati. Ninadhani Nyerere na Kaunda waliweka shinikizo katika serikali ya Nordic. “
Tore Linné Eriksen, msomi na mwanaharakati wa Norway.