SISI TUNAWEZA KUJIFUNZA KUTOKA KWA MARAFIKI WEMA.

Nchi za Nordic zina jumla ya watu milioni 27 tu, huku Pato lao kwa mwaka ni Dola za Marekani trilioni 1.7; (Dola za Marekani Bilioni 1700.)

  • Tanzania ambao idadi ya watu ni milioni 55, mara mbili zaidi ya nchi za Nordic, Pato la Taifa kwa mwaka jana lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 56.99.
  • Pato la nchi za Afrika lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 2.334.
  • Pato la mtu mmoja ni wastani wa Dola za Marekani 62,963. Lakini kwenye nchi za Afrika ni wastani wa Dola za Marekani 1,945

Rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amefungua mkutano wa 18 wa nchi marafiki za Afrika na Nchi za Nordic uliofanyika jijini Dar es Salaam Leo. amesema kwamba

Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweeden; licha ya kuwa na eneo dogo (kilomita za mraba milioni 3.5) na idadi ya watu wapatao milioni 27 tu; zina uchumi mkubwa. Pato lao kwa mwaka jana (2018) lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 1.7.

Kwa upande wa Afrika, Bara ni kubwa (lina kilomita za mraba milioni 30.37) na idadi ya watu wapatao bilioni 1.2. Hata hivyo, kwa mwaka jana 2018, Pato la nchi zote za Afrika lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 2.334.

Huku Tanzania ikiwa imebarikiwa na uwezo, fursa na mazingira ya kuingia kwenye ushirikiano madhubuti wa kiuchumi yapo

 “Kusema kweli, sisi Waafrika tuna jambo kubwa la kujifunza. Kwa sababu, wakati nchi za Nordic zenye jumla ya watu milioni 27 tu, Pato lao kwa mwaka ni Dola za Marekani trilioni 1.7; sisi Tanzania ambao tuko milioni 55, mara mbili zaidi ya nchi za Nordic, Pato letu la Taifa kwa mwaka jana lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 56.99 tu.” Amefafanua Rais Dk Magufuli

Lakini hata ukilinganisha Pato la mtu mmoja mmoja katika nchi za Nordic na Afrika, tofauti ipo kubwa sana. Kwa mfano, ukigawa Pato la nchi za Nordic la Dola za Marekani trilioni 1.7 kwa watu milioni 27, maana yake pato la mtu mmoja ni wastani wa Dola za Marekani 62,963. Lakini kwenye nchi za Afrika ni wastani wa Dola za Marekani 1,945.

Tofauti hii ni kubwa sana; hivyo basi, sisi Waafrika ni lazima tujitafakari ili tujue tunapokosea na tujifunze kutoka kwa marafiki zetu wa nchi za Nordic.

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AMTEUA BALOZI WILBERT IBUGE KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi (Kanali) …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.