- Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma imesema Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) haliwezi kufutwa tena kutokana na mwenendo wa sasa kuridhisha kutokana na utendaji wake na kubadili mtazamo wa awali.
- Kubadili kwa mtazamo huo kunatokana na mwenendo wa awali kutoridhisha katika utendaji wake hali iliyopelekea baadhi ya wabunge kutaka Shirika hilo lifutwe lakini leo tarehe 17/11/2019 wajumbe wa kamati hiyo wamesema kwa sasa shirika hilo haliwezi kufutwa tena kwa sababu juhudi nyingi za makusudi zimefanyika na kuna mambo yanaonekana na kamati imejionnea.
- “Sisi Wazaramo tuna msemo wetu “seeing is believing”, tukimaanisha kuwa kuona ni kuamini nilichokiona leo kwenye mgodi huu nadiriki kusema nimeona na nimeamini, na kwamba hata yale tuliyokuwa tunayasikia au kuyasoma ni tofauti sana na hiki tulicho kiona hapa” alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma Zaynabu Matifu Vulu
- ”Hata mimi nilikuwa mmoja wa wabunge niliokuwa ninataka STAMICO ifutwe lakini leo hapa nafuta kauli yangu na kwamba nimeona na nimeani na kwamba nimeridhishwa na kuna mambo yanafanyika yenye tija” alisema mjumbe Maftaha Nachuma.
- Waziri wa Madini akiwa na watendaji wake wa STAMICO na STAMIGOLD aliwaeleza wajumbe wa kamati kuwa STAMICO ya miaka miwili iliyopita ni tofauti na STAMICO ya sasa. STAMICO hii haizalishi madeni badala yake imekuwa ikilipa madeni, kuzalisha kwa faida na imefanikiwa kupunguza ghara za uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
- Aidha, Biteko amewaeleza wajumbe wa kamati kuhusu Changamoto mbalimbali zinazo isumbua STAMICO ni pamoja ya matumizi ya mafuta ya diesel kwa ajili ya kuzalisha umeme unaotumika mgodini hapo ambapo kwa mwezi wanatumia bilioni 1 wakati wangetumia umeme wa Tanesco wangekuwa wakitumia umeme kwa gharama ya milioni 300 kwa mwezi na kwamba wangekuwa wanaokoa Tsh milioni 700 kila mwezi.
- Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge wakichangia mjadala ulioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Dkt. Raphael Chegeni sehemu kubwa wameipongeza Wizara na STAMICO kwa mageuzi makubwa na kwamba kazi yao inatia moyo.
- Hali hiyo ilipelekea wajumbe kuiuliza STAMICO nini wanataka kamati hiyo iwasaidie ili kufikia malengo yao kama shirika kutokana na mipango yao waliyowaeleza wajumbe hao.
- “Ndugu wajumbe kwanza nimefurahishwa kuona mgodi huu ukiendeshwa na watanzania wenyewe na kwamba hili linatia moyo na kujivunia kwamba tuna uwezo wa kuanzisha miradi mingine mikubwa na ikaendeshwa na watanzania wenye, hiki ni kielezo kikubwa, nawapongeza sana”. Alisema Mwenyekiti wa Kamati.
- Aidha, mwenyekiti wa kamati alisema ni ukweli kwamba Waziri wa Madini Doto Biteko anaitendea haki nafasi aliyopewa na kwamba kuwekuwa na mabadiliko makubwa yanayo onekana kutokana na utendaji wake kamati inampongeza na iko teyari kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake huku pia akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwase.
Ad