TAASISI NNE ZATII AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUZITAKA KAMPUNI, TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA KUTOA GAWIO NA MICHANGO SERIKALINI NDANI YA SIKU 60

  • Siku moja baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa muda wa siku 60 kwa wenyeviti wa bodi na watendaji wa Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 pamoja na yale ambayo Serikali ina hisa kutoa gawio na michango yao kwenye mfuko Mkuu wa Serikali lasivyo wangepoteza nyadhifa zao, taasisi 4 zimetoa gawio na michango kwa Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dodoma leo jioni
  • Taasisi zilizotoa gawio ni pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambacho kimetoa shilingi bilioni 1 nukta 2, Shirika la Reli (TRC) Sh. bilioni 1, Shrika la Posta Tanzania (TPC) sh. milioni 350 na Mfuko wa SELF-Microfinance shilingi milioni 200 na kufanya jumla ya kiasi kilichopokelewa kuwa shilingi bilioni 2 nuta 75
  • Jana Mheshimiwa Rais Magufuli alipokea gawio na michango mbalimbali ya sh. trilioni 1.05 kutoka kwa Kampuni, taasisi na mashirika 79 kati ya 266 yaliyotakiwa kutoa gawio na michango hiyo huku taasisi 187 zikikwama kufanya hivyo.
  • Hatua ya taasisi hizo nne kutoa gawio na michango yao leo imefikisha gawio na michango iliyopokelewa na Serikali katika mwaka wa Fedha 2018/2019 kufikia sh. trilioni 1.325 huku kampuni 183 kukabiliwa na rungu la Waziri wa Fedha na Mipango kama hawatatekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kuwataka watendaji na Bodi zao kutoa fedha za gawio na michango ndani ya siku 59 zilizobaki.Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *