MADIWANI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA NAMNA YA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HALMASHAURI YA KINONDONI.

  • Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro jana walifanya ziara ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
  •  Madiwani hao waliokuwa wameambata na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Regina Chonjo, Mstahiki Meya  Amir Nondo wamepokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, Mstahiki Meya Benjamini Sita.
K1-01
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wakifuatilia uwasilishwaji wa namna ya ukusanyaji mapato.
  • Aidha madiwani hao pia wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo , Katibu Tawala Stela Msofe  pamoja na watumishi wengine wa Idara na vitengo ambapo pamoja na mambo mengine walipata nafasi ya kutembelea miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi bilioni 8.9.
  • Awali kabla ya kutembelea miradi hiyo , madiwani hao walipata nafasi ya kujifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato zilizotolewa na Msimamizi wa Mapato wa Halmashauri ya Kinondoni Zahoro Rashidi.
K2-01
Mhatshiki Meya wa Halmsahauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita katikati mwenye shati lakijani, wa kwanza kustoto ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Morogoro Amir Nondo, wakiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mjini Mh. Regina Chonjo wapili kulia na wa kwanza kulia ni Katibu wa tawala wa Kinondoni Bi Stela Msofe.
  • Akizungumzia ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Morogoro Mhe. Nondo alisema kuwa wamekuja kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato kwakuwa Halmahauri ya Kinondoni  imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukusanyaji.
  • “ Tumekuja kujifunza namna ya ukusanyaji mapato, ukiangalia kwenye takwimu zetu sisi tuponyuma, sasa leo tumekuja kuona wenzetu mnafanyaje hadi mnafikia malengo, wote ni wamoja tunategemeana ,tunaomba mtupatie ujuzi mliokuwa nao” alisema Mhe. Nondo.
K3-01
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh. Regina Chonjo akizungumza na madiwani, watendaji wa halmashauri za Kinondoni na Morogoro walipokuja kwenye ziara ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato. Wa kwanza kushoto ni Mstahiki Meya wa Morogoro Amir Nondo na Mstahiki Meya Benjamini Sita wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
  • Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Chonjo alisema aliishukuru Manispaa ya Kinondoni kwakuwapokea vizuri na kueleza kuwa wamefurahishwa na ukarimu waliopata kutoka kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo.
  • “ Lengo letu na kuja hapa ni kujifunza, tunawshukuru mmetukaribisha , undugu tuliouanzisha hapa isiwe mwisho, karibuni na nyinyi Morogoro, hili tunalolifanya ndio lile linalotakiwa na Rais Dk. John Magufuli, asanteni kwa ushiikiano wenu” alisema Mhe. Chonjo.
K4-01
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na madiwani , watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro walipofanyaziara jana kwa lengo la kujinza namna ya ukusanyaji mapato. Wengine ni Meya wa Halmashauri ya Morogoro wa kwanza kushoto Amir Nondo na wapili ni Benjamini Sita.
  • Akiwakaribisha Madiwani hao, Mstahiki Meya . Mhe. Sita alisema kuwa Halmashauri ya Kinondoni ipo vizuri kwenye  ukusanyaji wa mapato na kwamba anawakaribisha ili waweze kujinza kwa lengo la kutimiza adhma hiyo.
  •  Naye Mhe. Chongolo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa ilikufikia malengo ,viongozi hawana budi kuweka juhudi nania ya dhati katika kutekeleza majukumu yao na kwamba kila mmoja anapaswa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza wajibu wake.
K6-01
Afisa biashara wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Pastor akiwaelekeza jambo madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuhusu mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni.
  • “ Bila kuweka malengo ya dhati kabisa, tunaweza kufanya ziara za kujifunza tukamaliza maeneo yote, natusipae kitu, kikubwa ni kuweka nia, kama ilivyo kwa wenzetu wa kabila la hehe wakisema wanajinyonga basi wanajinyonga kweli, inamana waliweka nia , kwahiyo nasisi viongozi tuwaige wahehe katika kuweka nia ya kuleta maendeleo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KINONDONI YA TUMIA BILIONI 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *