MATUMIZI YA NISHATI MBADALA NI KITU CHA MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA – WAZIRI SIMBACHAWENE

  • Matumizi ya nishati ya kuaminika na endelevu ni kitu kisichoepukika kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kwa Taifa lolote duniani hasa tunapoelekea kufikia lengo la Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025. Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene alipokua akizindua maonyesho ya  14 ya kitaifa ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja ,  jijini Dar es Salaam.
33-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiwa pamoja na Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Bwana Jeroen Verheul wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja. Uholanzi ni Wafadhili wakubwa katika masuala ya nishati jadidifu.
  • Aliongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo  ni kuhakikisha kuwa masuala yote yanayokwamisha upatikanaji rahisi, ueneaji na ongezeko la matumizi ya Nishati hizi kwa wananchi wote hasa walioko vijijini na hata mijini linashughulikiwa ipasavyo.  ”Ninawashauri muwe tayari kupeleka huduma zenu vijijini kwa kuanzisha matawi ya biashara zenu huko  badala ya kunga’ng’ania mijini pekee” alisema Waziri Simbachawene.
11-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
  • Aidha alisititiza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inathamini juhudi  za uendelezaji  na uhamasishaji wa  matumizi ya Nishati jadidifu na udhibiti wa ubora wa vifaa na ufungaji wa mitambo mbalimbali, ili kuwa na Teknolojia endelevu katika ustawi wa Mazingira yetu. Pia amewaagiza TAREA kufanya utafiti kubaini kwa kiasi gani jamii ya Wananchi katika mkoa wa Dar es Salaam wanatumia nishati jadidifu.
  • “Naye Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Bwana Jeroen Verheul amemshukuru Waziri Simbachawene lakin pia amesema kuwa wataendelea kufadhili masuala mbalimbali  ya mazingira yakiwemo yanayohusu nishati mbadala kama ambavyo wamefanya kwa TAREA.
22-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene akiangalia taa inayotumia mwanga wa jua wakati akitembelea mabanda mbalimbali yaliyokuepo katika viwanja vya mnazi mmoja kwenye maonyesho ya nishati jadidifu.
  • Akiongea katika ufungzi huo Katibu wa Jumuia ya Nishati jadidifu Makamu Mwenyekiti wa TARE Bwana Prosper Magali, alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kufungua maonyesho hayo na aliongeza kuwa TAREA itaendelea kushughulika na  masuala ya nishati jadidifu lakini pia wanachukua maelekezo ya Waziri aliyowapa na kuyafanyia kazi.
  • Maonyesho hayo ya nishati jadidifu yameandaliwa na Jumuia ya nishati jadidifu (TAREA) ambapo hufanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu maonyesho hayo ymefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *