NAUMIA SANA KUONA BIDHAA AU KITU CHOCHOTE KINACHOHUSIANA NA SEKTA YA MADINI KIKIINGIZWA KUTOKA NJE – WAZIRI BITEKO

  • Upungufu wa madini ya Chumvi kwenye viwanda vya chumvi hapa nchini unamsikitisha waziri wa madini Doto Biteko kutokana na uwepo wa mahitaji (soko) makubwa ya wanunuzi wa madini hayo huku madini hayo yakiwa hayapatikani kwa wingi kutosheleza mahitaji kutokana na uzalishaji mdogo kutoka kwa wachimbaji wa madini hayo huku wanunuzi wakikosa madini hayo.
  • Akiongea leo tarehe 03/11/2019 ofisi kwake Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao chake na wamiliki wa kampuni wa viwanda vikubwa vya chumvi hapa nchini Neelkanth Lime anaemiliki; Neelkanth Lime (T) Ltd, Neelkanth Salt(T) Ltd na Rushabh Investment (T) Ltd, Biteko amesema, anasikitishwa na ukosefu mkubwa wa madini hayo huku akiambiwa kuwa kiasi kikubwa cha chumvi kinachotumika hivi sasa ni kutoka nje ya nchi kutokana uzalishaji mdogo uliopo hapa nchini.
2-01
3. Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini Prof. Shukran Manya akifafanua jambo kuhusu upatikanaji wa madini ya Chumvi hapa nchini mbele ya Waziri wa Madini Doto Biteko
  • “Siku zote huwa naumia sana kuona bidhaa au kitu chochote kinacho husiana na sekta yangu (Madini) kikiingizwa kutoka nje wakati uwezo wa upatikanaji wa kitu hicho upo hapa nchini. Kuna wakati tulilazimika kuzui uingizaji wa makaa ya mawe kutoka nje ili kuyapa nguvu masoko ya ndani na leo makaa yam awe yanathamani kubwa. Leo Madini ya Chumvi yanakosekana kwenye viwanda, niseme ukweli naumia sana moyoni.” Alisema Biteko.
  • Kwa upande wa uongozi wa Neelkanth Lime (T) wakiongozwa na Ahmed Said Meneja Mkuu akiwa na Rashid Ahmed Mkurugenzi ambao ni wanunuzi wakubwa wa madini ya nchumvi wamesema wanahangaika kupata idadi kubwa ya madini hayo ili kukidhi mahitaji yao hasa kwenye kiwanda chao kilichopo wilayani Mkuranga huku wakiwa wamepandisha bei ya kununua madini hayo hadi Tshs. 160,000/= kwa tani lakini bado mahitaji ni madogo.
  • “Mhe. Waziri tunahangaika sana kupata haya madini, sisi tumekwenda kila mahali, Lindi, Mtwara na hata hivi majuzi tulikuwa Tanga na tumefanya kikao na wazalishaji wa madini hayo kwenda kuongeza hamasa ya uzalishaji. Nikupe taarifa njema, kuanzia mwezi Februali mwaka huu kiwanda chetu kimeanza kuchakata tani 1000 kwa siku.” Alisema Rashid Ahmed.
3-01
Rashid Ahmed Mkurugenzi wa Neelkanth Lime akitoa maelezo na ufafanuzi kwa Waziri wa Madini Doto Biteko kuhusu upungufu wa Chumvi kwenye viwanda vyao
  • Ahmed, ameongeza kuwa mpaka sasa wastani wa 70% ya chumvi tunayoitumia ni kutoka nje kutokana na upungufu wa uzalishaji wa madini uliopo hapa nchini. Ameongeza kuwa wao wapo teyari kuwaweka wazilishaji wa chumvi kwenye vikundi vidogo vidogo waweze kuunganisha nguvu ili wazalishe kwa wingi huku wakiwawezesha kwa mikopo kama walivyo kufanya huko Mkuranga huku wakimiliki shamba lao la chumvi lenye hekari 2000.
  • Kutokana na kauli hiyo, kama kawaida Biteko kwa staili ile ile ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli “papo kwa papo” aliinua simu na kumpigia mwenyekiti wa Chama cha Wavunaji Chumvi Tanzania Habib Nour akitaka kuthibitisha kama kweli kuna upungufu wa uzalishaji wa madini ya chumvi na mwenyekiti huyo akapatikana na akamuwekwa “hewani” moja kwa moja mbele ya kikao.
  • Bila kung’ata maneno, Habib alikiri na kumwambia Waziri kuwa ni kweli kuna upungufu mkubwa wa uzalishaji wa madini ya chumvi hapa nchini huku juhudi za kimkakati wa kuongeza uzalishaji zinaendelea.
  • Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko ametoa wito kwa wachimbaji hasa wadogo kuongeza uzalishaji wao huku akiwasisitiza kukaa kwenye vikundi ili iwe rahisi kupata mikopo kwa ajili ya mtaji ili waweze kuzalisha na kukidhi mahitaji huku Neelkanth Lime(T) wakisema wako teyari kutekeleza ushauri uliotolewa na Waziri katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa mikopo kweye vikundi vyao.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

SOKO LA MDINI ULANGA LA KUSANYA MILIONI 396 NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *