MAZINGIRA SI KIKWAZO KWA WAWEKEZAJI – WAZIRI SIMA

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amesema Serikali imefanya mapitio ya Kanuni ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ili kurahisha uwekezaji nchi.
  • Akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika Mkutano  wa Mashauriano baina yao na Serikali katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani  Morogoro, Naibu Waziri Sima amesema gharama za kulipia vibali zimepungua na idadi ya siku  pia imepungua kutoka siku 145 mpaka siku 95 hivi sasa
22-01
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili kutoka kulia) akifuatilia majadiliano katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro. Kikao hicho kimelenga kutatua changamoto katika sekta ya uwekezaji takribani Mawaziri na Manaibu Waziri 13 wanashiriki kikao hiki.
  • “Ndugu zangu marekebisho haya yote yanayofanywa na Serikali, yanalenga kurahisisha mchakato wa tathmini ya Athari kwa Mazingira na kurahisisha uwekezaji hapa nchini, Mfano awali gharama kwa vituo vya mafuta zilikuwa zaidi ya Milioni kumi na kwa sasa gharama hizi zimepungua hadi kufikia Milioni Nne na nyingine Milioni mbili” Sima alisisitiza.
  • Katika hatua nyingine Naibu Waziri Sima, amesema Ofisi yake inaandaa Kanuni za Wataalamu Elekezi wa Mazingira ili kurahisisha uwekezaji kwa kuwa miradi yote ni lazima ipate cheti kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). “Tangu tumefanya mapitio ya Kanuni zetu, malalamiko kutoka kwa wawekezaji yamepungua kwa kiasi kikubwa sana” Sima alisisitiza
33-01
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akitoa ufafanuzi wa hoja zilizojitokeza katika Mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashra na Wawekezaji katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani Morogoro.
  • Hata hivyo Naibu Waziri Sima amewakumbusha washiriki wa Kikao hicho kuwa Mabadiliko ya tabianchi ni tatizo kubwa duniani, na kutoa rai  kwa  umma wa watanzania kupanda miti kwa wingi kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi. Amewaagiza wawekezaji hasa wenye Viwanda kuhakikisha wanaanzisha vitalu vya miche katika maeneo yao na kusisitiza kuwa ukaguzi wa masuala ya Mazingira katika maeneo yao utaanzia hapo
  • Mkutano huu wa Mashauriano baina ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji umelenga  kusikiliza na kutatua changamoto zao umefanyika leo  katika ukumbi wa Hoteli ya Glonency mkoani  Morogoro na kuendelea katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Jumla ya Mawaziri na Manaibu Waziri 13 wanashiriki Mkutano huu. Na Lulu Mussa Morogoro
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA KWA WAZALISHAJI NA WASAMBAZAJI WA MIFUKO ISIYOKIDHI VIWANGO – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *