WAZIRI HASUNGA – BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO NI MUHIMU KISEKTA

 

  • Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga amesema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni mkombozi kwa wakulima hapa nchini.
  • Mhe. Hasunga ameyasema hayo jana tarehe 9 Disemba 2019 alipotembelea na kukagua maghala ya kuhifadhi nafaka na katika eneo la Mkuyuni Jijini Mwanza.
4-01
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na mafundi wanaojenga uzio wa eneo linalozunguka kinu cha kukoboa mpunga kilichopo Mtaa wa Mkuyuni Wilaya ya Nyamagana wakati alipotembelea na kukagua maghala ya kuhifadhi nafaka Jijini Mwanza, jana tarehe 9 Disemba 2019.
  • Amevitaka bodi hiyo kuwa ni mkombozi kwa wakulima kutokana na jukumu lake la kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya nafaka unaongezeka kadhalika pia bodi hiyo inanunua mazao ya nafaka na kuyaongezea thamani.
  • Amesema kwa kuanzisha kiwanda Jijini Arusha cha kusaga nafaka na kuuza, huku kukiwa na dhamira ya  kujenga kiwanda cha kuchakata Alizeti na nafaka Jijini Dodoma itawanufaisha wananchi kwa kuuza bidhaa zilizotemgemezwa nchini tofauti na kuuza malighafi.
1-01
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Bi Monica Mbega kukagua maghala ya kuhifadhia nafaka yanayomilikiwa na Bodi hiyo Kanda ya Ziwa katika Mtaa wa Bohari Wilaya ya Nyamagana wakati alipotembelea akiwa katika ziara ya Kikazi ya siku moja Jijini Mwanza, jana tarehe 9 Disemba 2019.
  • Amesema kuwa dhamira ya serikali kupitia Bodi hiyo mkoani Mwanza ni kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga na mazao mengine hivyo bodi hiyo ni muhimu kisekta.
  • Mhe. Hasunga pia ameipongeza Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa kutekeleza vema maelekezo ya Serikali ya kununua na kuuza Korosho.
2-01
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua maghala ya kuhifadhia nafaka yanayomilikiwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Kanda ya Ziwa katika Mtaa wa Bohari Wilaya ya Nyamagana wakati alipotembelea akiwa katika ziara ya Kikazi ya siku moja Jijini Mwanza, jana tarehe 9 Disemba 2019.
  • “Moja ya Jukumu tulioipatia Bodi mwaka huu ni kununua na kuuza Korosho kwa niaba ya Serikali na kazi hiyo wameifanya vizuri, wameweza kunua Korosho yote na wanayo.” Alifafanua.
5-01
Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Bi Monica Mbega akimuonyesha Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) mpaka wa eneo la kinu cha kukoboa mpunga kilichopo Mtaa wa Mkuyuni Wilaya ya Nyamagana wakati alipotembelea na kukagua maghala ya kuhifadhi nafaka Jijini Mwanza, jana tarehe 9 Disemba 2019.
  • Alisema, Bodi kama wafanyabiashara imeweza kununua Korosho na kuongeza thamani (Ku- process) kwa kuziweka kwenye vifungashio vya viwango mbalimbali.Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mwanza

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 23 SKIMU YA UMWAGILIAJI NANGANGA WILAYANI RUANGWA KUWA IMEKAMILIKA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa siku 23 pekee kwa wakandarasi wanaojenga Skimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *