
- Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Joshua Nassari leo tarehe 11 Desemba,2019 ameongoza kundi la wafanyabiashara wapatao kumi kufika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
- Wageni hao wamefika kutoka jimbo la Hebei, China ambao wameonesha nia ya kuwekeza nchini kwenye miradi mbalimbali ya kuanzisha. Viwanda hivyo ni pamoja na kiwanda cha kuunganisha magari, kiwanda cha kutengeneza vioo vya milango na madirisha na kiwanda cha kutengeneza chakula.

- Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe amewakaribisha na kuwahakikishia utayari wa Serikali kuwasaidia kupata ardhi, vibali, leseni na vyeti vinavyotakiwa ili kufanikisha mipango yao ya uwekezaji nchini.
- TIC ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha, kuvutia na kusaidia wawekezaji wazawa na wageni kwa kuwa utekelezaji wa miradi hiyo, una matokeo makubwa yenye manufaa kwa Taifa na wananchi ikiwamo uzalishaji wa ajira.
Ad
Big up
Maendeleo hayana chama