MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU BANDARI YA KABWE MKOANI RUKWA WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 85

  • Ujenzi wa mradi wa miundombinu katika Bandari ya Kabwe mkoani Rukwa ambao unagharimu Sh.bilioni 7.498 tayari umekamilika kwa asilimia 85 na mkandarasi wa ujenzi huo ambaye ni Sumry’s Enterprises Ltd anatarajia kuukabidhi mradi huo Aprili mwaka 2020.
B-01
Mafundi wakiendelea na kazi ya kusuka nondo kwa ajili ya kutengeneza nguzo ambazo zitatumika kusimamisha gati ya bandari ya Kabwe.
  • Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Mradi wa gati ya Bandari ya Kabwe Usanifu na Ujenzi kutoka Sumry’s Enterprises Ltd William Shila amesema kuwa walipewa kazi ya ujenzi wa miundombinu hiyo ikiwemo ya gati, ofisi, majengo ya abiria pamoja na majengo mengine wezeshi Aprili 2 mwaka 2018 na kwa namna ambavyo kazi inakweda watakabidhi mradi kwa wakati.
  • Ameongeza kuwa utakapokamilika mradi huo utakuwa umesaidia kusogeza huduma ya usafiri wa meli karibu na wananchi wa Rukwa na maeneo yanayozunguka pamoja na nchi jirani ikiwemo ya DRC huku akieleza faida za sasa wakati ujenzi unaendelea ni kwa wananchi wa maeneo hayo kupata ajira kwani kila mwezi wanatumia Sh.milioni 30 kulipa wafanyakazi.
C-01
Mmoja wa mafundi akiendelea kuwajibika wakati wa ujenzi wa miundombinu ya bandari ya Kabwe iliyopo katika Ziwa Tanganyika upande wa Mkoa wa Rukwa.
  • Kuhusu changamoto ambayo wanakutana nayo kwenye ujenzi huo, amesema kubwa ni ya mawimbi ya maji ya ziwa kuwa makubwa kiasi cha kusababisha ujenzi kusimama mara kwa mara. “Changamoto yetu hapa ni hali ya hewa kwa maana mawimbi kuwa makubwa ya maji yanakwamisha kasi ya ujenzi huu, kwani kuna wakati tunalazimika kusimama na mawimbi yanapopungua tunaendelea na ujenzi.”
D-01
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa miundombin katika bandari ya Kabwe mkoan Rukwa.
  • Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano kwa uamuzi wake wa kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa kupewa kazi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwetu.”Tunaishukuru sana TPA kwa namna ambavyo imefungua fursa kwetu wazawa, miradi mingi ya bandari katika Ziwa Tanganyika inafanywa na Watanzania, tunashukuru kwa uamuzi wao wenye tija kwetu na kwa wananchi kwa ujumla.”
E-01
Baadhi ya mafundi wakiendelea na majukumu yao katika shughuli za ujenzi wa miundombinu katika Bandari ya Kabwe.
  • Awali Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama amesema mradi wa Bandari ya Kabwe ni mradi mkubwa kuwekezwa kwenye bandari za Ziwa Tanganyika na kwamba wenzao wa DRC wanafanya usafirishaji mkubwa wa shehena za mahindi na mchele, hivyo ni bandari muhimu na TPA iliamua kuweka fedha Sh.bilioni 7.498. Na Said Mwishehe, Michuzi Globu – Rukwa
Ad

Unaweza kuangalia pia

BANDARI YA KIWIRA LANGO KUU LA USAFIRISHAJI WA MIZIGO KATIKA ZIWA NYASA – MENEJA ABEDI GALLUS

Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii Imeelezwa kuwa Bandari ya Kiwira ni lango kuu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *