- Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) imesema imeshaweka miundombinu katika bandari za Ziwa Nyasa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa maeneo wanaozunguka ziwa hilo wanapata huduma ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda nyingine kwa kutumia usafiri wa majini zikiwemo meli.
- Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu , Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Abedi Gallus amesema katika bandari ya Itungi tayari kuna gati lenye urefu wa mita 70 , karakana na jengo la ofisi na katika bandari ya Kiwira kuna gati lenye urefu wa mita 15 la muda na ghala la kuhifadhia mizigo wakati bandari ya Mbamba Bay ina gati la muda mfupi .
- “Hata hivyo katika mwaka wa fedha 2019/2020 mamlaka imeshasaini mkataba wa ujenzi wa bandari ya Ndumbi wenye thamani ya Sh.bilioni 12.28 utakaotekelezwa kwa muda wa miezi 22.Katika bandari ya Liuli kuna jengo la ofisi na nyumba ya makazi wakati bandari ya Manda ina jengo la ofisi na nyumba ya makazi,”amesema Gallus.
Na Said Mwishehe,Michuzi Globu
- Hata hivyo amesema Mamlaka imesaini mkataba na kampuni ya Royal Haskoning HDV ya Uholanzi kwa ajli ya kufanya upembezi yakinifu, kuandaa michoro na kuandaa nyaraka za manunuzi kwa ajili ya kuendeleza Bandari za Ziwa Nyasa.
- Kuhusu vyombo vya majini, Gallus amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) inamiliki vyombo mbalimbali vya majini ambavyo vinaiwezeha mamlaka kutoa huduma zake kwa ufanisi. Amesema kuna meli mbili za mizigo ikiwemo ya MV.Ruvuma na MV.Njombe zenye uwezo wa kupakia shehena ipatayo tani 1,000 kila moja.
- “Meli ya moja ya abiria ya MV.Mbeya II ambayo ipo katika hatua ya majaribio na inatarajiwa kuanza safari zake ziwani mapema katika hatua ya mwezi wa Januari mwaka 2020.
Kwa upande wa vitendea kazi, amesema katika juhudi za kuhakikisha kuwa bandari za Ziwa Nyasa zinafanyakazi kwa ufanisi na tija, Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza kwenye vitendea kazi vya bandari kwa kununua vifaa. - Ametaja baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na mizani miwili yenye uwezo wa kupima hadi tani 100 kwa ajili ya kupima uzito mizigo inayohudumiwa katika bandari ya Ndumbi na Kiwira na kwamba mizani hiyo itawezesha mamlaka kujua kiasi halisi cha shehena inayopakiwa na kushushwa melini kwasabababu kulinda maslahi ya mamlaka na vile vile wateja wanaopitisha shehena bandarini kwa kulipa malipo yanayoendana na kiasi cha shehena kilichohudumiwa.
- Aidha bandari ina crane, folklift, karakana kubwa kwa ajili matengenezo ya magari na vifaa vingine vya bandarini.Pia amesema katika bandari za Ziwa Nyasa kuna jumla ya miradi mikubwa minne inayoendelea kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa fedha 2019/2020 ambayo inalenga kuboresha utoaji huduma.
Ad