RAIS DKT. SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA JENGO LA MICHEZANI MALL NA JENGO LA SHEIKH THABIT KOMBO

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa kulikuwa kuna kila sababu ya kufanyika Mapinduzi matukufu ya Januri 12, 1964 ili kuleta usawa na umoja sambamba na kuwafanya Waafrika waishi maisha bora.
  • Rais Dk. Shein aliyasema hayo  katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uwekaji wa mawe ya msingi ya Michenzani Mall na jengo la Sheikh Thabit Kombo, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square, Michenzani Mjini Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
4z-01
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na mkandarasi
  • Alisema kuwa Mapinduzi yameleta usawa, umoja, udugu na maelewano na kubwa zaidi ni kuondosha ubaguzi wa aina zote na kuwafanya watu wawe wamoja sambamba na kutandika mipango mipya ya maendeleo.
  • Rais Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar inayoonekana leo na ile ya miaka 60 iliyopita ni tofauti na hivi sasa kuna Zanzibar mpya iliyozaliwa Januari 12, 1964.
5z-01
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa mk
  • Akieleza historia ya Zanzibar, Rais Dk. Shein alisema kuwa wazee walipata madhila na hawakuwa na maisha mazuri kama ilivyo hivi sasa na kuwataka Wazanzibari kutosahau historia yao ikiwa ni pamoja na kujua walikotoka, walipo na wanakokwenda.
  • Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza historia ya mji wa Zanzibar na mipaka yake kabla ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 na jinsi Waafrika walivyokuwa wakiishi katika nyumba zisizostahiki kuishi binaadamu.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *