DKT. NDUGULILE ATAKA TAARIFA UTOAJI WA DAWA HOSPITALI YA RUFAA IRINGA

N1-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akisikiliza taarifa ya mkoa kutoka kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Iringa kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.
  • Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga kuhakikisha anapata taarifa ya utoaji wa dawa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
  • Agizo hilo limekuja mara baada ya ziara ya yake mkoani humo alipotembelea hospitali hiyo kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kushuhudia mmoja wa mama aliyejifungua Hospitalini hapo kupewa dawa mara moja badala ya mara tatu kama iilivyoandikwa na Daktari.
N2-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na kuzungumza na Bibi aliyekutana naye akipatiwa huduma katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • Dkt. Ndugulile amesema kuwa amekasirishwa na utendaji kazi wa manesi katika wodi ya Mama na Mtoto kwa kutozingatia utoaji huduma hasa kuhakikisha wazazi na watoto wanapewa dawa kwa wakati zinazotakiwa na kwa idadi sahihi.
N3-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua wodi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • Ameongeza kuwa lengo la mgonjwa kupewa huduma ni kuhakikisha anapona na sio kufanya aendelee kupata tabu na shida hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza fedha nyingi katika kuhakikisha Sekta ya Afya inaboreshwa nchini.
N5-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua maabara katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • “Haiwezekani mgonjwa kanunua dawa zake kwa fedha zake lakini bado hata hamzingatii kumpatia dawa mnategemea ataponaje” alisema Dkt. Ndugulile.
  • Aidha Dkt. Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kuhakikisha wanaratibu utoaji wa huduma hospitalini hapo ili kuepukana na malalamiko ya wagonjwa na kupoteza imani ya wananchi kwa Hospitali hiyo.
N6-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua maabara katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • “Tukiendelea hivi tutaondoa imani kwa wananchi wetu katika utoaji wa huduma za afya sisi tunatakiwa kutoa huduma kwa wananchi na sio kuwapa kero wananchi” alisema Dkt. Ndugulile.
N7-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua nyaraka mbalilmbali wakati alipotembelea kukagua stoo ya dawa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Atupele Mwandiga amemuahikikishia Naibu Waziri Dkt. Ndugulile kusimamia utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na kusimamia vilivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma inayostahili.
N8-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia mfuko unatumikia kuweka unga lishe unaotengenezwa na Kiwanda cha Ruaha Milling mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya tano imetoa kiasi cha Billioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya na maboresho katika Zahanati na vituo vya Afya mkoani humo katika kuhakikisha inaboresha Sekta ya Afya hivyo watasimamia Sekta hiyo kikamilifu.
N9-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimpima mtoto uzito katika siku ya lishe katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • “Mhe. Naibu Waziri tutahakikisha hatutopoteza imani ya wananchi katika utoaji huduma za afya na tutatendea haki rasimali fedha tulizopewa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Afya Mkoani kwetu” alisema Dkt. Atupele
  • Wakati huo huo Dkt. Ndugulile ametembelea na kujionea utendaji kazi utoaji wa huduma kwa wananchi katika Ofisi ya Bima ya Afya (NHIF), Kampeni ya masuala ya Lishe, Kiwanda cha Ruaha Milling na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo.
N10-01
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akishiriki kupika uji lishe kwa ajili ya watoto katika katika siku ya lishe katika eneo la Tanangozi mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.
  • Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile yuko katika ziara ya siku mbili mkoani Iringa kukuagua shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii mkoani humo.

 

 

 

 

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *