BODI YA USHAURI YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (MAB) KWA TMDA, YATEMBELEA OFISI YA TMDA KANDA YA ZIWA

  • Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(MAB) imefanya ziara maalum na kujionea mambo mbalimbali ya utendaji kazi katika ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).
  • Katika ziara hiyo, Bodi hiyo imeweza kujionea utendaji kazi za udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika maabara kubwa nacya kisasa iliyojengwa kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.
  • Aidha, bodi hiyo imeweza kufanya kikao chake cha kawaida, ikiwa ni cha kwanza kwa mwaka 2020.

T2-01

  • Sambamba na hilo Bodi imekutana na watumishi wa TMDA kanda ya Ziwa ambapo Mwenyekiti wa MAB, Mhe. Balozi, Dkt. Ben Moses amewapongeza Menejimenti naxwatumishi kwa mafanikio ya utendaji kazi yaliyofikiwa na kuwahimiza kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuwezesha taasisi kufikia lengo lake la kuendelea kulinda afya ya wananchi kwa ufanisi zaidi.
  • Ziara ya wajumbe wa MAB inahusisha pia kutembelea na kujionea changamoto za udhibiti katika vituo vya Forodha vya Sirari na Mutukula.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *