RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM AKITOKEA MAPUMZIKONI CHATO MKOANI GEITA

1-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dart es salaam mara baada ya kuwasili akitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari 9, 2020
  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 09 Januari, 2020 amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita.
  • Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli kesho ataanza ziara ya kikazi Visiwani Zanzibar ambako ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.
2-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dart es salaam mara baada ya kuwasili akitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari 9, 2020
  • Keshokutwa (11 Januari, 2020), Mhe. Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni.
  • Rais Magufuli atashiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili tarehe 12 Januari, 2020 katika uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi.
4-01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari 9, 2020
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *