BALOZI SEIF: JUKUMU LA WATOTO WA SASA NI KUSOMA KWA BIDII ILI KUENDELEZA DHANA YA MAPINDUZI

  • Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Watanzania wanapoadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar lazima wale walioshuhudia wajikumbushe wakati kile Kizazi Kipya kinapaswa kusoma Historia ili kujua vyema dhamira iliyopelekea kufanywa kwa Mapinduzi hayo.

Z2-01

  • Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Bwejuu mara baada ya kuzindua Majengo Mawili ya Skuli ya Charity {Madrasa na Dakhalia ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za Maadhimisho ya kutimia Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
  • Balozi Seif ameleza kwamba kazi inayowakabili kwa sasa Watoto wote ni kusoma kwa nguvu zao zote katika malengo ya kwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia yaliyoikumba Dunia kwa wakati huu.

Z3-01

  • Akitoa Taarifa ya Kitaalamu ya Mradi huo wa Kijamii Katibu Mkuu Wizara ya Eimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Dk. Idriss Muslim Hijja amesema zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Mia 682,000,000/- zimetumika kugharamia Mradi huo Mkubwa.
  • Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi kawenye hafla hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma amesema Ujenzi wa Dakhalia ni Moja ya Mikakati bora inayowajengea Wanafunzi kupata muda wa ziada wa kujisomea.
  • Mradi wa Skuli ya Charity Bwejuu ulioanzishwa na Wananchi wenyewe Mnamo Mwaka 2014 ukianza na Wanafunzi 25 ulilenga kuwarejesha masomoni Watoto walioacha Skuli, Watoto yatima pamoja na Watoto wenye Mahitaji Maalum, ikiwemo pia Futari wakati wa Mwezi wa Ramadhani kwa Wazee wasiojiweza.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *