- Seriakli imezidi kubana mianya ya wiza wa mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za mitaa kwa kukabidhi mashine za kukusanyia mapato kwa njia ya kielektroniki 7227 zenye mfumo madhubuti wa kudhibiti wadanganyifu kucheza na mashine hizo.
- Zoezi la kukabidhi mashine hizo zenye muonekano unaofanana na utambulisho wa Serikali wakati zinapowashwa na kuzimwa limefanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Mhe. Seleman Jafo Jijini Dodoma mapema kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote 185.
- Akikabidhi mashine hizo Jafo aesema kuna watu walikua wanaendelea na ujanja wa kudukua mifumo ya mashine zilizokuwa zinatumika kukusanya mapato ikiwemo kubadili tarehe na na kuzima internet ili fedha hizo zisisomeke kwenye mfumo wa Serikali.
- Aliongeza kuwa mashine za awali zilikuwa rahisi katika kubadiri baadhi ya taarifa ndiyo maana wameamua kuja na mfumo mwingine unaokwenda kuzuia kabisa wizi huo.
- “Sasa mwisho wa udanganyifu wa naman hii umekwisha kwanza mashine hizi tumeziagiza wenyewe na kuweka mfumo tunaotumia sisi na hauruhusu kubadilisha tarehe wala kuzima internet hivyo chochote kitakachotokea kwenye mashine hiyo kitaripotiwa na kubainika mara moja” alisema Jafo.
- Hata hivyo, Jafo alisema licha ya baadhi ya halmashauri kuwa na makusanyo makubwa, lakini anapata kichefuchefu kuona wanashindwa kujenga hata na matundu ya vyoo vya walimu katika maeneo yao.
- “Tunakwenda kuziba mapengo ya wizi, lakini kuna watu wanakatisha tamaa kwani hadi mwishoni wa desemba mwaka jana, hawakuwa wamefikia hata asilimia 20 ya malengo ya makusanyo wakati wengine walikuwa zaidi ya asilimia 50,” alisema Jafo.
- Akizungumzia kuhusu mashine hizo, alisema zinakwenda kuongeza idadi kwani awali kulikuwa na mashine 10,100 katika halmashauri zote nchini hivyo kwa sasa kutakuwa na mashine 17,327 ambazo zitapelekea halmashauri kuwa na uwezo wa kukusanyo juu zaidi.
- Jafo aliongeza kuwa mashine hizo ni kipimo kwa wakurugenzi kama wanatosha au hawatoshi lakini pia alisema mwezi April mwaka huu atamkabidhi Rais majina ya wote ambao anapendekeza wachukuliwe hatua baada ya kuonesha kushindwa kutimiza majukumu yao.
- Katika hatua nyingine Waziri amesema kuna wakurugenzi wengi wanafanya kama wanavyotaka wao hali iliyopelekea baadhi ya halmashauri kushindwa kulipa hata posho za madiwani, akasema kuna halmashauri zinadaiwa na madiwani Sh 758 na akakabidhi taarifa hiyo kwa Katibu Mkuu Eng. Nyamuhanga ili aweze kuifanyia kazi.
- Upatikanaji wa mashine hizo 7227 zimepatikana kupitia msaada wa Norway ambapo Balozi wa Norway nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen alisema nchi yake imetoa msaada huo baada ya kuzingatia uhusiana na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
- Jacobsen alisema makusanyo ya Tanzania yatapanda kulinganisha na awali lakini akasema mashine hizo zimetengenezwa kwa tejknolojia ya hali ya juu hivyo si rahizi kudukuliwa.
- Katibu Mkuu wa OR- Tamisemi Eng. Joseph Nyamhanga amesema mashine hizo kila moja ilinunuliwa kwa dola 140 ambazo ni sawa na shilingi 320,000 ambazo kwa jumla zimegharimu sh 3.2 bilioni wakati bei ya kawaida wangeweza kununua kwa thamani ya sh 6.5. Bilioni hivyo wameokoa zaidi ya Sh 4 bilioni.
- Nyamhanga alisema mashine hizo zina neno maalumu, rangi na haziruhusu kuweka mifumo mingine hata kubadirisha tarehe ambapo amesema njia hiyo ni ya kuwadhibiti wachakachuaji.
- Haya ni mafanikio makubwa kwa OR-TAMISEMI kuweza kukabidhi mashine hizi ambazo zitasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Ad