TAASISI YA MOYO YAPOKEA MSAADA WA MASHINE NDOGO YA KIGANJANI YA KUANGALIA JINSI MOYO UNAVYOFANYA KAZI Matokeo ChanyA+ January 23, 2020 Taarifa Vyombo vya Habari, Taarifa ya Habari, Tanzania MpyA+ Acha maoni 735 Imeonekana Mkuu wa kitengo cha cardiovascular radiology ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasiya Kifai akiangalia mashine ndogo ya kiganjani (V-Scan dual) ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram), kupima mishipa ya damu na ultrasound ambayo Taasisi hiyo imepewa msaada na kampuni ya Computech30.Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 22 itatumika kwa wagonjwa walioko wodini na wakati wataalamu wa Taasisi hiyo watakapokwenda kwa wananchi kutoa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo (Outreach program) Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea msaada wa mashine ndogo ya kiganjani (V-Scan dual) ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram), kupima mishipa ya damu na ultrasound kutoka kwa Sandip Datta ambaye ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Computech30.Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 22 itatumika kwa wagonjwa walioko wodini na wakati wataalamu wa Taasisi hiyo watakapokwenda kwa wananchi kutoa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo (Outreach program) Ad Share Facebook Twitter Stumbleupon LinkedIn Pinterest