DIPLOMASIA YA TANZANIA YAZIDI KUIMARIKA

  • Mara kadhaa tumekua tukiona Rais Dkt. John Magufuli akiwaapisha mabalozi wateule ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni.
  • Katika miaka mitano ya uongozi wake, Rais Magufuli ameteua jumla ya mabalozi 42 na Mabalozi wadogo watatu hivyo kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya wawakilishi 45 kati ya mataifa 195 yanayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.
  • Kwa wale tunaojua hesabu za kugawanya, tutagawa 195 ÷45 na kupata wastani kuwa Balozi mmoja anaziwakilisha jumla ya nchi 4 jambo linaloungwa mkono na wadau wa Diplomasia na Maendeleo. Idadi hiyo haijajumuisha Mabalozi wa Heshima waliopo sehemu mbalimbali wanaoiwakilisha nchi yetu nje.
  • Idadi hiyo inatokana na kuongeza jumla ya mabalozi nane katika nchi ambazo hapo awali hazikua na uwakilishi kutoka Tanzania. Mataifa hayo ni: Cuba, Korea Kusini, Israel, Qatar, Sudan, Algeria, Namibia, na Uturuki.
  • Mabalozi hao wameteuliwa kimkakati kwa kuzingatia manufaa watakayoyapata watanzania katika mataifa hayo. Mfano: mwaka 2019 vijana 100 wa kitanzania walikwenda Israel kujifunza kilimo chenye tija huku Tanzania ikipokea maelfu ya watalii kutoka kwenye taifa hilo la Mashariki ya Kati.
  • Pia, Mabalozi hao wamekua Wagunduzi wa fursa za masomo, biashara, na nyenginezo zinazopatikana kutoka kwenye mataifa ya nje.
  • Mungu Ibariki Afrika! Mungu Ibariki Tanzania! Mungu mbariki Rais Wetu Mh.Dr. John Pombe Magufuli. Ameeen

Patrick Joseph Paul
Diaspora- Uturuki

Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE DKT. NDUMBARO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI TANO HAPA NCHINI

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.