- Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa walezi wa kwanza kwenye jukumu la kumlea mtoto.
- Mheshimiwa Shonza ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Mgeni Jadi Kadika (CUF) lilikokuwa likisema serikali haioni sasa ni wakati muafaka kwa vijana wetu kuwekewa umri maalumu wa kutumia mitandao ili kupunguza mmomonyoko wa maadili.
- Akijibu swali hilo la msingi Mhe.Shonza alisema kuwa ni kweli utandawazi umechangia sana katika kuleta mmomonyoko wa maadili kwa kiasi kikubwa kwa jamii zetu hususani vijana kupitia intaneti,mitandao ya kijamii na maudhui ya nje kupitia muziki na filamu na ndiyo maana serikali ilileta Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrime Act) ya Mwaka 2015 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Mtandao na Maudhui ya Redio na Runinga za Mwaka 2018.
- ‘’Serikali iliiona changamoto hii mmomonyoko wa maadili na ndiyo maana ikaunda Sheria hiyo ambayo ilipigiwa sana kelele ndani na nje ya nchi kuwa ibana uhuru ,‘’alisema Shonza.
- Mhe.Shonza akiendeleza kuzungumza wakati ajibu swali la hilo alisisitiza kuwa familia na wazazi ndiyo wenye jukumu la ujumla la kumlea mtoto na taasisi za elimu ya awali,Msingi,Sekondari hadi Elimu ya Juu ambao huwaelimisha kwa maneno na vitendo watoto na vijana kuhusu utambuzi wa mambo mema na mabaya yanayofaa na yasiyofaa, na baada ya hatua hizo ndipo wajibu mkubwa wa serikali unapojitokeza.
- Akiendelea kujibu swali la nyongeza la mbunge huyo lilihoji je, serikali haioni haja kufanya kama nchi zilizoendelea kuzuia watoto kuingia katika mitandao na kuangalia picha chafu katika mitandao,Naibu Waziri huyo alijibu kwa kusema kuwa serikali imekwisha fanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuunda sheria zinazosimamia masuala hayo, hivyo alitoa wito kwa viongozi kuwa wakwanza kuzisimamia sheria hizo na alisisitiza kuwa suala la malezi ya watoto siyo la serikali peke yake bali ni pamoja na wazazi.Na Anitha Jonas – WHUSM
Ad