NATOA WITO KWA WAZAZI KUTOWARUHUSU WATOTO KUREJEA CHINA MPAKA PALE SERIKALI ITAKAPOJIRIDHISHA NA HALI INAVYOENDELEA NCHINI HUMO – WAZIRI MKUU

1-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma, Januari 30, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wazazi wenye watoto wanaosoma nchini China kutoruhusu watoto hao kurudi nchini humo kwasasa mpaka pale Serikali itakapotoa tamko baada ya kupata taarifa kutoka kwa Balozi wa Tanzania Nchini China Mbelwa Kairuki  kuhusu hali inavyoendelea nchini humo kufuatia ugonjwa unao sababishwa na kirusi cha CORONA.
  • Waziri Mkuu amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali liloulizwa na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi lilotaka kujua Serikali imejipangaje kukabiliana na kudhibiti ugonjwa huo kwa Tanzania kufutia muingiliano wa kibiashara baina ya Tanzania na China.
  • Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeimarisha mawasiliano kati ya Serikali na ubalozi wake nchini China na ubalozi wa China  hapa nchini ili kupata taarifa za namna hali inavyoendelea nchini humo zitakazo saidia kutoa taarifa kwa wanafunzi hao kurejea nchini humo kuendelea na massomo yao hali ya ugonjwa huo itakapopungua.
4-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2020. Kulia ni Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Jaku Ayoub. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
3-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Katimba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2020 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Momba, David Silinde kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, Januari 30, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2-01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma, Januari 30, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA BODI YA NHC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *