ZANZIBAR NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA YA UTALII

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uwamuzi wa busara na wenye tija wa Angola wa kutaka kushirikiana na Zanzibar kwenye sekta ya utalii hatua ambayo itaimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo.
  • Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa Angola katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sandro Agostinho de Oliveira aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais.
  • Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuusifu na kuupongeza uwamuzi huo wa Angola wa kutaka kushirikiana na Zanzibar katika sekta ya utalii na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni chachu ya maendeleo kwa pande mbili hizo.
  • Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Oliveira kuwa Zanzibar na Angola zina mambo mengi ya kushirikiana kwa pamoja ambayo yanaweza kuleta mafanikio makubwa kwa pande zote mbili yakiwemo mashirikiano katika sekta ya utalii.
  • Dk. Shein alieleza kuwa uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na Angola ni njia moja wapo kubwa itakayopelekea kuimarika zaidi kwa sekta ya utalii ambapo Zanzibar imepiga hatua kubwa..
  • Aidha, Dk. Shein alimueleza Balozi Oliveira kuwa Zanzibar na Angola zote kwa pamoja zina mambo mengi ya kujifunza kwa kila upande ikiwa ni pamoja na namna ya kuendeleza na kuimarisha sekta ya utalii.
  • Alisema kuwa kwa upande wa Zanzibar sekta ya utalii ni nguzo kubwa ya uchumi ambayo imekuwa ikichangia kiasi cha asilimia 20 ya Pato la Taifa na asilimia 80 ya fedha za kigeni.
Ad

Unaweza kuangalia pia

BALOZI SEIF: JUKUMU LA WATOTO WA SASA NI KUSOMA KWA BIDII ILI KUENDELEZA DHANA YA MAPINDUZI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Watanzania wanapoadhimisha Miaka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.